Monday, 26 December 2016

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA SONGWE TAREHE 21 DISEMBA, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akiongea na wajumbe wa kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Songwe .






Katika kikao hicho Wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ngazi ya Halmashauri za Wilaya waliwasilisha taarifa mbalimbali ili zipitiwe na kupatiwa ushauri na kwa ajili ya utekelezaji.

Baadhi ya maswala yaliyojadiliwa na kupitishwa ni haya;
kwamaba Mkoa kuunda Tume ya kufuatilia na kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mbozi na Songwe. 
Kwamba eneo lililojengwa Chuo cha Ufundi kwa msaada wa nchi ya Japani ambacho kinatarajiwa kusimamiwa na VETA lipimwe na kupatiwa hati miliki mapema.
Kamati ilikubaliana kuwa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe zijengwe katika eneo la kijiji cha Selewa


No comments:

Post a Comment