Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akiwa katika ziara zake
za kawaida kutembelea Halmashauri za wilaya za Songwe alitembelea wilaya ya
Mbozi tarehe 16 Disemba, 2016 ambapo alikutana na Wakuu wa Idara kwa lengo la kuwabadilisha kifikra ili waweze kupanga
mikakati ya kuongeza kipato cha Wananchi tofauti na utaratibu uliozoeleka
Chiku Gallawa hakuridhishwa na taarifa
zilizokuwa zinatolewa na Wakuu Idara kwa
sababu hazikuwa na takwimu sahihi. Vilevile jinsi walivyozoea kufanya kazi, alisema “Wataalam msing’ang’anie kufanya vitu ambavyo havitoi matokeo ambayo serikali
inategemea wapate wananchi”. Alisisitiza.
Alishauri Wataalam wafunguke kwa kusoma wengine wanafanya
nini.
Aliagiza kila Idara iandae mkakati ya Idara katika wiki moja na kuwakilisha kwake
kupitia kwa mkuu wa Wilaya.
Vilevile aliagiza kuwa Watumishi wa Idara ya Maendeleo ya
Jamii, Kilimo, Mapato waende vijijini ili warudi ili waandae mikakati yao.wapangiwe
kata ili kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wanachi na kwamba shughuli za
uratibu wa miradi zifanyike kutoka katika kata.
Upande wa Mazingira alisema Mtaalam anayeratibu kitengo
hicho ameshindwa kusimamia ipasavyo hivyo
alimwagiza Mkurugenzi ampangie kazi nyingine.
Aidha aliongeza kuwa hati chafu katika Wilaya ya Mbozi
inatokana na wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea.
Vilevile aliagiza kuwa NGO zote zitambuliwe katika
Halmashauri na kujua shughuli zao pamoja na bajeti ili kutorudia kazi ambazo
Halmashauri inatekeleza.
No comments:
Post a Comment