Tuesday 22 August 2017

Ziara ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya M. Ntandu kwenye miradi ya Mkoa


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya M. Ntandu akitembelea mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa katika eneo la Selewa , Mbozi tarehe 22 Agosti, 2017




~

Sunday 6 August 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA TANZANIA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

Waziri wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiongea na Wananchi katika Viwanja vya  Halmashauri ya Wilaya ya Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi tarehe 20 Julai, 2017

Mheshimiwa Waziri Kassim Majaliwa akikagua mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Naming'ongo , Wilaya ya Momba  tarehe 21 Julai,2017



Waziri Mkuu Majaliwa akisimikwa kuwa chifu wa Wanyamwanga kutoka kwa Chifu Chipanzyamakandi Mkoma wa VI  katika kijiji cha Makamba kilichopo katika Halmashauri ya Momba tarehe 21 Julai, 2017

Waziri Majaliwa akizindua ujenzi wa OPD ya Hospitali ya Wilaya ya Ileje tarehe 21 Julai,2017

Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha Taarifa wakati wa uzinduzi wa Zoezi la uandikishaji tarifa za Wakazi kwa njia ya Kieletroniki na kwamba zoezi hilo  limeanzia katika Wilaya ya Mbozi

ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI SONGWE

Na mwandishi wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe kuanzia tarehe 20 – 24/07/2017.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali. katika Wilaya ya Momba alitembelea mradi wa umwagiliaji wa Naming’ongo, Ujenzi wa nyumba za Watumishi na kuzindua zoezi la upimaji ardhi na kutoa Hati za Kimila. Halmashashauri ya mji wa Tunduma Mradi wa Kituo cha pamoja cha ushuru wa Forodha (One Boarder Stop Post – OSBP), Ileje alizindua ujenzi wa OPD. Kuzindua daftari la Wakazi la Kieletroniki (ambalo litatumika kuanzia ngazi ya kitongoji, na  kuzindua kitabu cha Rasimu ya Mkoa wa Songwe.
Katika majumuisho alisema haya
Ulinzi na usalama
Wananchi waendelee kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wa wananchi katika mapambano dhidi ya mauaji ya wazee, Walemavu wa ngozi – Albino, ulevi uliokithiri wa Viroba, mila zilizopitwa na wakati za kunyima haki wanawake na watoto
Pembejeo Feki
Alikemea swala la usambazaji wa pembejeo feki na kuwa serikali hitafumbia macho na alitaka ushirikiano ili kudhibiti usambazaji wa pembejeo feki
Aiongeza kuwa pembejeo zenye ubora  zisambazwe kwa wakati.  Uchumi
Waziri Majaliwa alisema kuwa Serikali itaendea kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu
Uhakika wa chakula
 Waziri aliwataka Wananchi wahakikishe wanakuwa na uhakika wa chakula kwa kupanga bajeti ya mavuno ili kuepukana na balaa la njaa
Upimaji wa ardhi
 Wazari Mkuu alitoa shukrani kwa mkoa wa Songwe kuzingatia umuhimu wa ardhi kwa kuanza  kupima ardhi yake ili iongeze thamani na kuwa na matumizi bora ya ardhi – kilimo, mifugo, hifadhi ya misitu, hifadhi ya wanyama pori na kuwa hilo litapunguza migogoro isiyo ya lazima.
Afya
 Wazir Majaliwa alisisitiza umuhimu wa kuboreshewa huduma za Afya – Mama Wajawazito na Watoto

Elimu
Kutokana na serikali kutoa huduma za elimu bure Waziri aliagiza ujenzi wa shule za ufundi ili kuongeza  ajira ya vijana
 Vile vile kila shule ianzishe madarasa ya awali ambayo yatatumika kuwaandaa  watoto wa miaka minne hadi mitano kabla ya kujiunga na darasa la kwanza.
Akijibia changamoto la uhaba wa Waalimu Waziri Majaliwa alisema serikali imetoa   vibali vya ajira kwa watumishi 10,184 kuziba pengo la Watumishi Feki, na vibali vingine 52,436 ambapo katika idadi hiyo wamo Watumishi wa Sekta ya Elimu.
Utalii
Waziri mkuu aliagiza kuwa Vivutio vya utalii viboreshwe na kutangazwa ili kuongeza vyanzo vya mapato.
Ulevi
Waziri Mkuu Majaliwa alikemea tabia ya ulevi na kuzuia usambazaji na matumizi ya pombe aina ya Viloba.
Hali ya ulinzi na Usalama mipakani
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alitoa  agizo kuwa waliojenga nyumba ndani ya mita 50 kutoka mpaka wa Tanzania na Zambia wabomoe  wenyewe katika muda wa siku.
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea mpaka huo aliagiza Halmashauri kuweka alama kwenye nyumba 250 ambazo zilibainika kuwa ndani ya eneo huru (No man’s land) zinatakiwa kubomolewa kwa muda usiozidi miezi mitatu.




Thursday 16 March 2017

MKUU WA WILAYA SAMWEL JEREMIAH APOKEA MABATI KUTOKA KAMPUNI YA SBSMk

Mkuu wa Wilaya Samwel Jeremiah akipokea mchango wa mabati kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya SBS Eliona Sabaya katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe. 

Na Sia Kisamo

 Samwel Jeremiah akipokea mchango huo wa mabati 250 alitoa shukrani kwa meneja huyo wa kampuni ya Camp of Small business Solution (SBS) iliyopo Mkwajuni Songwe kuwa mchango huo utachangia kukamilisha  ujenzi katika Sekta za Elimu, Afya pia Ulinzi na Usalama hususan kituo cha Polisi. Halitmaye aliwataka Wadau wengine waige moyo huo wa kutoa michango mbalimbali ili kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Songwe.



MKUU WA WILAYA YA SONGWE AKAGUA MRADI WA NYUKI MBANGALA


Tuesday 14 March 2017

MKUU WA WILAYA YA SONGWE ATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WALIOFANYA VIZURI


Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah akitoa zawadi kwa wafafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidatu cha  Tatu kuingia cha  Nne.

Mkuu wa Wilaya katika picha ya pamoja na wanfunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana kuingia kidato cha tano,
wanafunzi hao waliahidiwa na mkuu wa Wialya kupatiwa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama motisha na kuwafanya waendelee kufanya vizuri katika masomo yao

Mkuu Wilaya katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha tatu kungia kidato cha nne  wa shule ya sekondari Ifwenkenya


Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Ifwenkenya

Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya elimu kata ya Ifwenkenya