Thursday, 16 March 2017

MKUU WA WILAYA YA SONGWE AKAGUA MRADI WA NYUKI MBANGALA

Samwel Jeremaiah akiongea na Wafugaji Nyuki


Mkuu wa Wilaya  Samwel Jeremiah akiwa na Wafugaji nyuki pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya


 Mkuu wa Wilaya aridhishwa na Mradi wa Nyuki 

Na mwandishi wetu Sia Kisamo


Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah alitembelea mradi wa wafugaji nyuki katika kitongoji cha Njira Kata ya Mbangala
Mkuu wa Wilaya hiyo alizungumza na kikundi hicho chenye wanachama 30 na Mizinga iliyofungwa mpaka sasa ni 150. Aidha Mkuu wa Wilaya aliwaahidi kuwapatia Mabati 32 ili kumalizia banda la pili la kufugia nyuki ambalo hapo awali aliwapatia mbao.  Vileville aliwasisitiza wafugaji hao  kuhakikisha wanajiunga na mfuko CHF kwa ili kuwa na uhakika wa matibabu ya afya zao.


No comments:

Post a Comment