Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah akiongea na Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Maweni
Mkuu wa Wilaya akiwa katika picha ya pamoja Walimu na Wanafunzi
Na Sia Kisamo: Afisa Utamaduni Songwe
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah akiwapongeza wanafunzi
wa Shule ya sekondari Maweni kidato cha sita kwa kufanya vizuri katika
mashindano ya Mock Mkoa wa Songwe ambapo shule hiyo ilishika nafasi ya nne
kimkoa kati ya shule 12 zilizoshiriki mashindano ya mitihani hiyo. Mkuu wa
Wilaya aliwatia moyo Waalimu na wanafunzi na kuwaambia Waalimu waongeze
juhudi katika ufundishaji na wanafunzi wajitahidi kusoma kwa bidii na
kuzingatia masomo.
Pia Mkuu wa Wilaya hiyo alisema wanafunzi waliofanya vizuri na
kushika nafasi ya kumi bora wanaandaliwa zawadi na kuwaahidi kuwa wanafunzi
watakaofanya vizuri zaidi katika mtihani wa Taifa watapata nafasi mbili za
kusoma USA na China.
No comments:
Post a Comment