Monday 29 August 2016

Kikao cha kazi cha wataalam wa Mkoa wa Songwe


Washiriki wa kikao cha kazi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakati wa kufunga kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa  wa Sogwe  iliyopo Vwawa Mbozi tarehe 26 Agosti, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa alifanya kikao  cha kazi na Maafisa Utamaduni, Maendeleo ya Jamii, Habari, TEHAMA na ushirika kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe uliopo Vwawa Mbozi.

Lengo la mkutano huo ilikuwa kupanga mikakati namna ya kuwakwamua vijana katika dimbwi la umaskini. Afungua kikao hicho mkuu wa mkoa alisema Vijana wengi wanatumia muda wao mwingi kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali badala yake hutumia muda huo kwenye ulevi, michezo ya pool na shughuli zisizo na tija.

Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa "nimewaita ili mjadili kwa pamoja namna ya kuandaa mikakati ya kuwatao vijana hawa ili kuiwezesha Tanzania kuingia katika kundi la mataifa yenye uchumi wa kati kufikia 2025". aliongeza kuwa ni muhimu kuwatambua vijana wasio na kazi, wananojishughulisha, na kuelimisha umuhimu wa vikundi ili iwe rahisi kupata mikopo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuongeza ubora wa bidhaa ili kuingia katika soko la ushindani

vilevile alitoa ahadi ya Gari kwa timu ya wilaya itakayokuwa ya kwanza kuhamasisha na kufanikisha uanzishwaji wa kiwanda katika eneo lao kutoka kwenye vikundi au wadau wa maendeleo.

Hatimaye, Mkuu wa Mkoa alitoa vitendea kazi vya mawasiliano (Ipad) kwa Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Sia Kisamo na Alfred Simpoli Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.




Mwenyekiti wa kikao cha kazi akiwasilisha majumuisho ya kikao hicho kwa Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa tarehe 26 Agosti, 2016


Sunday 28 August 2016

KIKAO CHA KAZI NA WATAALAM MKOA WA SONGWE TAREHE 26 AGOSTI,2016

Mkuu wa  Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akimkabidhi Ipad Afisa TEHEMA  wa wilaya ya Momba Alfred Simpoli  baada ya kikao cha kazi kilichohusu namna ya kuwakomboa vijana kiuchumi  katika Mkoa wa Songwe.



Mkuu wa  Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akimkabidhi Ipad Afisa Utamaduni wa wilaya ya Songwe Sia  baada ya kikao cha kazi. 


SIKU YA USAFI MKOA WA SONGWE TUNDUMA TAREHE 27 AGOSTI, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Songwe akifanya usafi katika eneo la Kilimanjaro Tunduma tarehe 28 Agosti, 2016


Wananchi wakitanya usafi katika eneo la kata ya Majengo

Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishirikiana  na wananchi kufanya usafi katika eneo la Kituo cha Mabasi kikuu kilichopo  katika kata ya Majengo



Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Modest Mkude (mwenye kofia) akiongea na wanachi baada ya kufanya usafi katika eneo la gulio la Iboya lililopo katika kata ya Majengo


Afisa Tarafa ya Tunuduma Edward Lugongo akiongea na Wananchi

Shughuli za usafi zikiendelea katika eneo la kata ya Tunduma


Mkuu wa Mkoa akipata maelekezo ya usafi wa mji wa Tunduma kutoka kwa Mtendaji wa Kata ya Tunduma Mohamed Kaguo

Siku ya usafi katika Mkoa wa Songwe iliyanyika Tunduma tarehe 27 Agosti,2016


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akihamasisha wananchi umuhimu wa kuweka mji wa Tunduma katika hali ya usafi. alisema " Tunduma ni sehemu ya mapokezi ya wageni kutoka nchi mbalimbal hivyo panatakiwa kuwa pasafi muda wote"

Akizungumza na wananchi wa eneo la Kisimani








aliongeza kuwa, yatafanyika majadiliano na wafanyabiashara wa kubadilisha fedha mikononi ili kurasimisha  biashara hiyo na kufanyika katika sehemu itakayotengwa na Halmashauri ya Mji kwa ajili ya usalama.




Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa kwa umakini

Thursday 25 August 2016

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SONGWE KATIKA WILAYA YA MOMBA

Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akivuka daraja la kuning'inia kutoka Kamsamba wilaya ya Momba kwenda Kilyamatundu wilaya ya Sumbawanga
Mto Momba ( picha ilipigwa juu ya daraja la kuning'inia la Kamsamba - Kilyamatundu)

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA TAREHE 22 - 23 AGOSTI, 2016

Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akivuka mto Momba baada ya kutembelea kijiji cha Kilyamatundu kilichopo katika Wilaya ya Sumbawanga
 Mtaalam wa Halmashauri Mhandisi wa Ujenzi akipima eneo la ujenzi wa nyumba ya Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Momba

Maandalizi ya mboga kwa ajili ya chakula baada ya kazi ya ujenzi wa msingi wa nyumba ya kituo cha Polisi cha Wilaya ya Momba
 Baadhi ya Watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakijiandaa kwa kazi ya kuandaa msingi wa nyumba ya kituo cha Polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa na Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando (katikati) wakisikiliza tafsiri ya ramani kutoka kwa mtaalam wa jeshi la Magereza tarehe 22 Agosti 2016
Majadiliano kuhusu ramani ya kituo cha polisi cha Wilaya ya Momba
Maandalizi ya kuchimba msingi wa nyumba ya kituo cha Polisi
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akiongeza nguvu kazi katika ujenzi wa msingi wa kituo cha Polisi
Mafundi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Magereza,  Mgambo, Halmashauri ya Wilaya na Wanakijiji wakishirikiana kujenga msingi wa nyumba ya Kituo cha Polisi
Mtaalam wa Magereza akipanga mawe kwenye msingi wa kituo cha polishi

ZIARA YA MKUU WA MKOA KATIKA WILAYA YA MOMBA



Ujenzi wa Msingi wa Kituo cha Polisi cha Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe yaliyopo katika kijiji cha Chitete, Kata ya Chitete Tarafa ya Msangano tarehe 22 Agosti, 2016

Friday 5 August 2016

ZIARA YA WAZIRI WA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MHE. GEORGE SIMBACHAWENE (MBUNGE) KATIKA MKOA WA SONGWE.



Waziri George Simbachawene na Mkuu wa Mkoa wakielekea Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuongea na Watumishi.
Waziri akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Aloyce Tuwoneye Mdalavuma

Ziara ya Waziri wa Ujennzi, Uchukuzi na Mawasilano Prof. Makame Mbalawa Mkoani Songwe. 



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbalawa amesema hakubaliani na hali ya ujenzi wa jengo la kupokelea wageni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Songwe na hivyo kuahidi kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na thamani halisi ya fedha iliyotumika na taratibu za kumpata mkandarasi aliyejenga.

Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Songwe alipofanya ziara ya siku moja kuwa hajaridhika na hali ya jingo lilivyo licha ya serikali kutoa fedha nyingi huku jingo hilo likiwa halijakamilika na mkandarasi hayupo katika eneo la kazi kwa muda mrefu.

Alisema  miundombunu ya ujenzi wa majengo katika uwanja huo hakubaliani nayo wakati uwanja ukiwa umejengwa vizuri na kuwa serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ujenzi unakamilika na ndege kubwa zikiwemo za mizigo zianze kutua ili kusaidia kusafirisha mizigo ya wakulima na hivyo kuinua uchumi wao.

“Tumejenga vizuri barabara ya kurukia ndege lakini tunashangaa hatua ua jingo hilo hairidhishi na siko tayari kulipokea hadi hapo nitakapojiridhisha” alisema Mbalawa
Alisema kufuatia hali hiyo serikali itaunda timu ya kufuatilia namna mkandarasi huyo alivyopatikana, thamani halisi ya fedha ikijiridhisha ndipo itakapotoa fedha za kumalizia ujenzi huo ili huduma ziendelee.

Waziri huyo alisema kwa kuzingatia umuhimu wa miundombinu ya mawasiliano sasa serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasaidia wananchi ambao wanapata shida kwa kutenga asilimia 46 ya bajeti ya mwaka 2016 hadi 2017 ambayo ni sawa ni zaidi ya Sh. 1.2 tilioni zikiwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa  miundombinu.

Kwa upande wake meneja wa uwanja wa Songwe Hamisi Amiri alisema mkandarasi wa kwanza ambaye ni kampuni ya Kundasighn aliacha kuendelea na ujenzi hali ambayo imesababisha kutokukamilika kwa wakati.

Alisema kwa sasa kuna kampuni nyingine ya Shamphrey ambao wameanza kujenga miundombinu ya majengo ambapo hadi sasa mkandarasi huyo hajalipwa kiasi chochote cha pesa hali inayosababisha kzi ya ujenzi kuendelea kusuasua.

Stephano Simbeye, Mwananchi
simbeyesjmwananchi@gmail.com
Watumishi ngazi ya Mkoa na Halmashauri wakimsikiliza Waziri.

 Ziara ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Mkoani Songwe

Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya pembejeo kwa Waziri.

Hali ya afya ya udogo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inadaiwa kuzidiwa na tindikali nyingi, hivyo kuwa chanzo cha kushuka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali na hivyo kuwakosesha tija wakulima.

Hayo yameelezwa jana na wadau na watafiti katika shamba la Mbegu la Mbozi lililopo eneo la Magamba mkoani Songwe kwa Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi Dkt. Charles Tizeba kuwa hali ya udongo imekuwa kikwazo kutokana na kuwa licha ya kutumia mbolea za chumvi chumvi lakini hazitoi matokeo mazuri kwa mkulima.

Robert Hamisi ni mtaalamu wa uzalishaji mbegu kutoka Kampuni ya Meru alisema kuwa katika eneo la hekta 220, uzalishaji ulikuwa tani 2.5 hali iliyofanya washituke na kuomba ushauri kwa Kampuni ya Yara ambao walifika shambani hapo na kuchukua sampuli ya udongo na kwenda kupima maabara nchini Norway.

Alisema baada ya kupata majibu ya kipimo cha udongo walishauriwa aina ya mbolea ya kutumia ili kurejesha afya ya udungo inayoongeza virutubisho vilivyopotea na sasa mwaka huu mavuno yameongezeka na kwamba wamelipa hekta 310 wanatarajia kuvuna tani 1320 ikiwa ni ongezeko kubwa.

Akizungumzia suala la afya ya Udongo Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba kujua hali ya udongo ni jambo la muhimu ili kuwafanya wakulima wasiendelee na kilimo cha kubahatisha na kuahidi kufanya kila jitihada ili kusaidia sekta ya kilimo.

Alisema alizungumza na wataalamu wa udongo kutoka kituo cha utafiti Uyole ambao wamemweleza kuwa ardhi ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inakabiliwa na udongo kuwa na tindikali nyingi hivyo kufanya mbolea za chumvichumvi kutokuwa na tija, hata hivyo alisema wanaweza kutumia chokaa kupunguza hali hiyo.

Hata hivyo alisema kutokana na kuwa katika mkoa wa Songwe madini hayo ya chokaa yanapatikana kwa wingi wataalamu watafika kukagua kama ndiyo yanayofaa kwa ajili ya kupunguza tindikali hiyo ya udongo ili wakulima waweze kuitumia kutibu udongo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa akizungumza katika kituo cha uzalishaji Mbegu Magamba alikitaka kituo hicho kuongeza ubunifu ili kuweza kuwezesha wakulima wadogo wadogo kujifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji wa mbegu na elimu nyingine ili kueneza teknolojia ambayo itasaidia kupunguza tatizo la kuuziwa mbegu bandia.

Alisema wakulima wa mkoa wa Songwe wana uwezo mkubwa wa kulima lakini wanakwamishwa na changamoto ambazo hata hivyo zikisimamiwa vizuri zinaweza kutatulika na kuwa kitendo cha mbegu kusafirishwa kwenda kusindikwa Mbeya kinahamisha ajira za wakazi wa eneo hilo na ni kinyme cha mkakati wa mkoa kuanzisha viwanda ili malighafi zinazozalishwa ziweze kusindikwa katika eneo husika.

Awali katika taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji kiongozi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Firmin Mizambwa pamoja na kuwa afya ya udongo kuwa tatizo linalopunguza ufanisi wa uzalishaji lakini pia wakala huo unakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ukosefu wa umeme wa grid ya taifa ambao unasababisha mbegu zinazozalishwa hapo kusafirishwa hadi Mbeya kwa ajili ya kusindikwa hali ambayo inaongeza gaharama.

Mizambwa aliongeza kuwa pia wanakabiliwa na tatizo la wananchi kuvamia shamba na uharibifu wa misitu ikiwa ni pamja na mifugo kuingia kiholela kwenye shamba.

Stephano Simbeye, Mwananchi
simbeyesjmwananchi@gmail.com

Waziri akipata maelezo ya uzalishaji miche bora ya Kahawa kutoka kwa Mtafiti Mkufunzi Charles Mwingira katika kituo cha Utafiti wa Kahawa TACRI Mbozi.
Waziri Dkt. Charles Tizeba akitoa uzoefu wake kuhusu zao la Kahawa