Monday, 29 August 2016

Kikao cha kazi cha wataalam wa Mkoa wa Songwe


Washiriki wa kikao cha kazi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakati wa kufunga kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa  wa Sogwe  iliyopo Vwawa Mbozi tarehe 26 Agosti, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa alifanya kikao  cha kazi na Maafisa Utamaduni, Maendeleo ya Jamii, Habari, TEHAMA na ushirika kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe uliopo Vwawa Mbozi.

Lengo la mkutano huo ilikuwa kupanga mikakati namna ya kuwakwamua vijana katika dimbwi la umaskini. Afungua kikao hicho mkuu wa mkoa alisema Vijana wengi wanatumia muda wao mwingi kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali badala yake hutumia muda huo kwenye ulevi, michezo ya pool na shughuli zisizo na tija.

Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa "nimewaita ili mjadili kwa pamoja namna ya kuandaa mikakati ya kuwatao vijana hawa ili kuiwezesha Tanzania kuingia katika kundi la mataifa yenye uchumi wa kati kufikia 2025". aliongeza kuwa ni muhimu kuwatambua vijana wasio na kazi, wananojishughulisha, na kuelimisha umuhimu wa vikundi ili iwe rahisi kupata mikopo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuongeza ubora wa bidhaa ili kuingia katika soko la ushindani

vilevile alitoa ahadi ya Gari kwa timu ya wilaya itakayokuwa ya kwanza kuhamasisha na kufanikisha uanzishwaji wa kiwanda katika eneo lao kutoka kwenye vikundi au wadau wa maendeleo.

Hatimaye, Mkuu wa Mkoa alitoa vitendea kazi vya mawasiliano (Ipad) kwa Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Sia Kisamo na Alfred Simpoli Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.



No comments:

Post a Comment