Thursday 16 March 2017

MKUU WA WILAYA SAMWEL JEREMIAH APOKEA MABATI KUTOKA KAMPUNI YA SBSMk

Mkuu wa Wilaya Samwel Jeremiah akipokea mchango wa mabati kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya SBS Eliona Sabaya katika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe. 

Na Sia Kisamo

 Samwel Jeremiah akipokea mchango huo wa mabati 250 alitoa shukrani kwa meneja huyo wa kampuni ya Camp of Small business Solution (SBS) iliyopo Mkwajuni Songwe kuwa mchango huo utachangia kukamilisha  ujenzi katika Sekta za Elimu, Afya pia Ulinzi na Usalama hususan kituo cha Polisi. Halitmaye aliwataka Wadau wengine waige moyo huo wa kutoa michango mbalimbali ili kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Songwe.



MKUU WA WILAYA YA SONGWE AKAGUA MRADI WA NYUKI MBANGALA


Tuesday 14 March 2017

MKUU WA WILAYA YA SONGWE ATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WALIOFANYA VIZURI


Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah akitoa zawadi kwa wafafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidatu cha  Tatu kuingia cha  Nne.

Mkuu wa Wilaya katika picha ya pamoja na wanfunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana kuingia kidato cha tano,
wanafunzi hao waliahidiwa na mkuu wa Wialya kupatiwa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama motisha na kuwafanya waendelee kufanya vizuri katika masomo yao

Mkuu Wilaya katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha tatu kungia kidato cha nne  wa shule ya sekondari Ifwenkenya


Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Ifwenkenya

Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya elimu kata ya Ifwenkenya



Friday 10 March 2017

MKUU WA WILAYA YA SONGWE ARIDHISHWA NA UFAULU WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MAWENI

 Mkuu wa Wilaya ya Songwe  Samwel Jeremiah akiongea na Wanafunzi wa  shule ya sekondari ya Maweni


Mkuu wa Wilaya akiwa katika picha ya pamoja Walimu na Wanafunzi 

Na Sia Kisamo: Afisa Utamaduni Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah akiwapongeza wanafunzi wa Shule ya sekondari Maweni kidato cha sita kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Mock Mkoa wa Songwe ambapo shule hiyo ilishika nafasi ya nne kimkoa kati ya shule 12 zilizoshiriki mashindano ya mitihani hiyo. Mkuu wa Wilaya aliwatia moyo  Waalimu na wanafunzi na kuwaambia Waalimu waongeze juhudi katika ufundishaji na  wanafunzi wajitahidi kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo.
Pia Mkuu wa Wilaya hiyo alisema wanafunzi waliofanya vizuri na kushika nafasi ya kumi bora wanaandaliwa zawadi na kuwaahidi kuwa wanafunzi watakaofanya vizuri zaidi katika mtihani wa Taifa watapata nafasi mbili za kusoma USA na China.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA WILAYA YA SONGWE







Kikundi cha Utamaduni cha akina  Mama kikitoa burudani

Mkuu wa Wilaya ya Songwe ashindwa kuvumilia ajumuika na umati kuselebuka


Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Wilayani Songwe  Machi 8, 2017.

Na Sia Kisamo: Afisa Utamaduni Songwe


Maadhimisho hayo yalifanyika katika kata ya Kanga Wilayani Songwe. Mgeni rasmi katika maazimisho hayo alikua Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah, katika maazimisho hayo Mkuu wa Wilaya  alisisitiza usawa na haki ambazo binadamu yeyote anapaswa kupewa, pia alisema kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni "Tanzania ya viwanda, wanawake ni misingi ya mabadiliko ya kiuchumi" kauli mbiu hiyo ipo kwa sababu serikali inaona umuhimu wa wanawake katika shughuli za kiuchumi,hivyo katika kufanya kazi fursa sawa zitolewe kwa wanawake na wanaume kwa sababu ndiyo msingi wa maendeleo nchini. 





MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA AZINDUA UPANDAJI MITI WILAYANI SONGWE


Mkuu wa Mkoa wa Songwe azindua zoezi la upandaji miti Wilaya ya Songwe  tarehe 03/03/2017

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe akizindua zoezi la upandaji miti Wilaya ya Songwe uliofanyika katika shule ya msingi Kaloleni iliyopo Kata ya Mkwajuni. 
Jumla ya miti 595,827 inatarajiwa kupandwa kwa mwaka huu Wilayani humo ambapo kwenye uzinduzi huo jumla ya miti 1000  ilipandwa na wananchi wa kijiji cha kaloleni wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa 

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Songwe Mhe. Abraham Sambila akiungana na Mkuu wa Mkoa katika zoezi hilo



Wananchi wa kijiji cha kaloleni wakishiriki katika zoezi la upandaji miti. 

Na Sia Kisamo; Afisa Utamaduni Songwe


Katika zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliwasisitiza wananchi kupanda miti maeneo ya shambani na nyumbani na kuongeza kuwa kila shule na Taasisi zote ziwe na bustani ya miche isiyopunguwa 2000 ili wanafunzi waweze kujifunza na kupeleka elimu hiyo kwa wazazi wao na kwa ajili yao wenyewe wakianza maisha yao. kampuni ya Mgodi wa Dhahabu ya shanta imeahidi kununua miche hiyo.
 Aidha, Mkuu wa Mkoa alisisitiza uwepo wa chakula mashuleni baada ya kuhojiana na wanafunzi wawili walio onekana bado hawajapata chakula, Alisisitiza kuwa wazazi wahusike kuhakikisha watoto wanasoma na wanahudhuria masomo kwa wakati.  Mkuu wa Mkoa alisema "Mzazi ambaye mtoto wake hataenda shule atachukuliwa hatua, na pia mzazi ambae atashiriki kuozesha mtoto chini ya miaka 18 atachukuliwa hatua kali za kisheria" alisisitiza