Maadhimisho hayo yalifanyika katika kata ya Kanga Wilayani Songwe. Mgeni rasmi katika maazimisho hayo alikua Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah, katika maazimisho hayo Mkuu wa Wilaya alisisitiza usawa na haki ambazo binadamu yeyote anapaswa kupewa, pia alisema kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni "Tanzania ya viwanda, wanawake ni misingi ya mabadiliko ya kiuchumi" kauli mbiu hiyo ipo kwa sababu serikali inaona umuhimu wa wanawake katika shughuli za kiuchumi,hivyo katika kufanya kazi fursa sawa zitolewe kwa wanawake na wanaume kwa sababu ndiyo msingi wa maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment