Friday, 10 March 2017

MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA AZINDUA UPANDAJI MITI WILAYANI SONGWE


Mkuu wa Mkoa wa Songwe azindua zoezi la upandaji miti Wilaya ya Songwe  tarehe 03/03/2017

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe akizindua zoezi la upandaji miti Wilaya ya Songwe uliofanyika katika shule ya msingi Kaloleni iliyopo Kata ya Mkwajuni. 
Jumla ya miti 595,827 inatarajiwa kupandwa kwa mwaka huu Wilayani humo ambapo kwenye uzinduzi huo jumla ya miti 1000  ilipandwa na wananchi wa kijiji cha kaloleni wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa 

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Songwe Mhe. Abraham Sambila akiungana na Mkuu wa Mkoa katika zoezi hilo



Wananchi wa kijiji cha kaloleni wakishiriki katika zoezi la upandaji miti. 

Na Sia Kisamo; Afisa Utamaduni Songwe


Katika zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliwasisitiza wananchi kupanda miti maeneo ya shambani na nyumbani na kuongeza kuwa kila shule na Taasisi zote ziwe na bustani ya miche isiyopunguwa 2000 ili wanafunzi waweze kujifunza na kupeleka elimu hiyo kwa wazazi wao na kwa ajili yao wenyewe wakianza maisha yao. kampuni ya Mgodi wa Dhahabu ya shanta imeahidi kununua miche hiyo.
 Aidha, Mkuu wa Mkoa alisisitiza uwepo wa chakula mashuleni baada ya kuhojiana na wanafunzi wawili walio onekana bado hawajapata chakula, Alisisitiza kuwa wazazi wahusike kuhakikisha watoto wanasoma na wanahudhuria masomo kwa wakati.  Mkuu wa Mkoa alisema "Mzazi ambaye mtoto wake hataenda shule atachukuliwa hatua, na pia mzazi ambae atashiriki kuozesha mtoto chini ya miaka 18 atachukuliwa hatua kali za kisheria" alisisitiza



No comments:

Post a Comment