Meneja
wa Taasisi ya fedha ya Bayport kanda za juu kusini Emmanuel Nzutu (aliyevaa
shati jeupe wa nne kutoka kulia ) akimkabidhi Kompyuta Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe Wakili Elias Nawera.
BAYPORT WATOA KOMPYUTA MBILI KWA AJILI YA MATUMIZI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGWE
Na Sia Kisamo - Afisa Utamaduni Songwe
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe na kuhudhuriwa na baadhi ya Wataalam, Meneja wa Taasisi hiyo alisema kuwa, wanathamini utendaji wa Halmashauri kwa maendeleo ya wananchi ndiyo maana wameamua kutoa msaada wa Kompyuta mbili za mezani ili kurasisha utekeleza wake.
Naye Mkurugenzi wa Wilaya alitoa shukrani na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika nyanja mbalimbali ili kutimiza adhma ya serikali kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
|
No comments:
Post a Comment