Friday, 18 November 2016

MPANGO KABAMBE WA KURASIMISHA ARDHI KATIKA MKOA WA SONGWE

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa akizindua upigaji picha za anga  kwa kutumia teknolojia ya ndege ndogo bila rubani (Drone) kwa msaada wa COSTECH katika Kata ya Chapwa, Halmashauri ya Mji wa Tunduma  tarehe 17 Novemba, 2016.

Mkuu wa Mkoa akielezea mpango kabambe wa  upimaji na Urasimishaji ardhi katika Mkoa wa Songwe.    

 Chiku Gallawa alisema kuwa mpango huo ulianzia katika Halmashauri ya Tunduma chini ya MKURABITA  baada ya  kuona ongezeko la Watu ni kubwa na Tunduma ni sehemu ya kuingilia na kutokea   Wageni kutoka nchi za nje.  Aidha aliongeza kuwa upigaji picha  utasaidia kutambua majengo yaliyopo  na kufanya makadirio ya ukusanyaji wa kodi ya majengo kuwa rahisi. Aliongeza kuwa watu waliojenga kwenye vyanzo vya maji, eneo huru la mpaka watajulikana kwa urahisi hivyo kurahisisha namna ya kurekebisha maeneo hayo.  Mwisho aliwashukuru COSTECH kwa mchango wa kitaalam na Teknolojia wanayotumia kupima kwa muda mfupi na gharama ndogo.  

Mkuu wa Mkoa akipata maelezo ya namna ya kuongoza upigaji picha kwa kutumia kompyuta kutoka kwa Wataalam wa COSTECH 


Mkuu wa Mkoa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tundma Mheshimiwa Ally Mwafongo

Ziara ya kukagua shughuli za upimaji  ardhi kwa ajili ya kupanga matumizi ya Ardhi katika Kata ya Kapele, Wilaya ya Momba


Mkuu wa Mkoa akiongoa na Wananchi wa Kijiji cha Kapele umuhimu wa kupanga matumizi ya ardhi. 

Akiongea na wanakijiji hao alisema upangaji wa matumizi ya ardhi ukikamilika matumizi ya ardhi yatakuwa wazi na hakutakuwa na mianya ya rushwa kwa sababu kila kipande cha ardhi kitajulikana matumizi yake.  Aliongeza kuwa ardhi itaongezeka thamani  kwani hati ya kumiliki ardhi inaweza kutumika ili kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za fedha. pia aliwashukuru wanachi kwa ushirikiano wao na Wataalam wa Halmashauri .


 Wanakijiji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa 

Mkuu wa Mkoa akitembelea makazi ya muda ya Wapima Ardhi wa Wilaya ya Momba

Mtaalam Mpima wa ardhi  Kelvin  Tulyanje akimwonesha Mkuu wa Mkoa kazi inavyofyanyika  baada ya kuhamishiwa kwenye Kompyuta 


Saturday, 12 November 2016

SIKU YA UZINDUZI WA UPANDAJI MITI ULIOYOFANYIKA KIMKOA WILAYANI ILEJE


Siku ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa ulifanyika Katika Kijiji cha Ngulilo kilichopo katika kata ya Ngulilo wilayani Ileje tarehe 10 Novemba, 2016


Mkuu wa Mkoa akisamlimiana na Watumishi wa Halmashauri wa Wilaya ya Ileje

Mkuu wa Mkoa akiongea baada ya kusomewa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.         

Akiongoea baada  ya taarifa hiyo Chiku Gallawa alisema uharibifu wa mazingiara unafanya wananchi wasivune sawa na wanavyokeza. alisisitiza kuwa hakuna jinsi nyingine bali ni lazima kuandaa , kusimamia na kutekeleza mikakati ya kurejesha uoto wa asili. aliongeza " hatuhitaji serikali kutuletea misaada kwani tutaonekana tumeshindwa wakati sivyo"

  Mkuu wa Mkoa aliisifu halimashauri ya Ileje kuvuka lengo la kuotesha miche kwani imefikisha miche 1,080,000 wakati lengo la kila Wilaya ni kuotesha miche 1,500,000. 

Pia aliagiza kuwa kati ya miti inayooteshwa inatakiwa kuwa na miche ya miti ya matunda ili baadaye wilaya ziwe na matunda ya kutosha kutegemea  hali ya hewa ya za mazingira husika kwa kuzingatia ushauri wa Wataalam. 

 Pamoja na ushari huo alishangaa kuona kaya zingine zinalima mpaka karibu na kuta za nyumba zao bila kuona mti hata mmoja, hivyo aliagiza kuwa kila kaya ihakikishe inapanda miti karibu na nyumba zao.

UZINDUZI WA KUPANDA MITI KWENYE CHANZO CHA MAJI KILICHOHARIBIWA NA SHUGHULI ZA KILIMO CHA  MSITU WA SERIKALI WA NGULILO
Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akipanda mti kwenye chanzo cha maji cha msitu wa Ngulilo

Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara  Viongozi wa Siasa, Wanafunzi na Wananchi waking'oa mahindi katika eneo la chanjo cha maji cha Ngulilo.


MKUTANO WA KIJIJI BAADA YA KUPANDA MITI


Monday, 7 November 2016

ZIARA YA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI VICTORIA MWAKASEGE ALIPOTEMBELEA WILAYA YA ILEJE

Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akizungumza na baadhi ya  viongozi wa Wilaya ya  Ileje wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Isongole Ileje- Tanzania naMbilima Chitipa- Malawi. 

  Mkuu wa Wilaya ya Chitipa,Grace Chirwa akizungumza na baadhi ya watendaji wa Tanzania na Malawi wakati wa ziara ya kukagua mipaka. 


Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akiwa na watendaji wa wa nchi zote mbili katika mpaka wa Tanzania na Malawi. Mkuu wa kituo cha polisi cha Itumba -Ileje mkoani Songwe(kulia) Afande ASP Slivanus Mnubi akibadilishana mawasiliano na Mkuu wa Kituo cha polisi cha Chitipa-Malawi(kushoto) SOP Gray Chimphepo ikiwa ni sehemu ya kuthibiti uharifu mpakani.