KIKAO CHA KAZI NA PEMBEJEO CHA MKOA WA SONGWE
Kikao kazi na Pembejeo cha mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi tarehe 04 Novemba, 2016
Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akifungua kikao hicho, alisema kuwa watafiti wa chuo cha Dar es Salaam walifanya utafiti katika wilaya za Mbozi, Ileje na Momba walibaini kuwa hizi Wilaya zinaongoza kwa kusambaziwe pembejeo zenye ubora wa viwango vya chini ( Feki). Aliongeza kuwa takwimu za wafafiti hao zinaonesha kuwa wakulima wanapoteza 80% ya mapato watarajiayo. "Hatuwezi kuvumilia hali hii, tutahakikisha tunapanga mikakati itakayozuia usambazaji haramu huo" alisisitiza. vilevile alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wamenza kuingiza mbegu zenye ubora wa chini, wamekatwa na sheria imechukua mkondo wake. Mkuu wa Mkoa alifafanua kuwa pembejeo za ruzuku ni asilimia 3 ya mahitaji ya Mkoa, hivyo alishauri kuwa Viongozi na Wataalam wasiegemee upande wa asilimia 3 tu bali wahakikishe alimia 97 inayobakia inaratibiwa vizuri ili isiwe mwanya wa kuingizia pembejeo zenye viwango vya chini. Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa aliwaagiza wakurugenzi kuwa taarifa zote kutoka ngazi ya Halmashauri zao wazielewe na kujiridhisha kabla ya kuzipeleka nje ya wilaya zao na siyo kuwaachia wakuu wa Idara wazipitishe. Alisisitiza uhakika wa taarifa, Kufanya kazi kwa umakini, mwonekano maridadi, na ushirikiano utaifanya Songwe iende kwa kasi anayoitaka Mheshimiwa Rais.
Katibu wa Mkoa Eliya M. Ntandu akisisitiza umuhimu wa kutoa taarifa zilizo sahihi.
Kamanda wa Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mathias Nyange akieleza namna vyombo vya usalama vilivyojipanga kupambana na wasambazaji pembejeo zenye ubora wa kiwango cha chini.
No comments:
Post a Comment