Friday, 4 November 2016

MSAKO WA PEMBEJEO FEKI SONGWE WAZAA MATUNDA

Wafanya biashara watano wakamatwa wakiuza mbegu bandia

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu msimamo wa Mkoa kuhusu pembejeo bandia.

Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa mkoa hautarusu pembejeo zisizokidhi viwango hazitaruhusiwa  na Mfanyabiashara yeyote atayekamatwa na pembejeo bandia atachukuliwa hatua na vyombo vya sheria . Pia alisema kuwa  katika msimu huu wa Kilimo Wafanyabiashara Watano wamekamatwa kwenye Mji Mdogo wa Mlowo, Mbozi na hatua za kisheria juu yao zinaendelea juu yao.  Aidha, Mkuu wa mkoa alisema hatakubali kuona nguzu za wakulima alisilia 80 zinazopotea bure kwa kutumia pembejea zilizo chini ya kiwango.


Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe,  Kamishna Msaidizi wa Polisi  Mathias Nyange akionesha mifuko ya mbegu za Mahindi zilizokamatwa zikiwa na jumla ya kilo 455. Kamanda Nyange alisema Wafanyabiashara hao bado wanashikiliwa na Polisi, pia alisema Watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanywa kwa kushirikiana na Wataalamu wa mbegu kutoka Kampuni ya Pannar kwenye Mji Mdogo wa Mlowo.

Mkuu wa Mkoa akionesha mbegu zilizokamatwa




No comments:

Post a Comment