Friday 18 November 2016

MPANGO KABAMBE WA KURASIMISHA ARDHI KATIKA MKOA WA SONGWE

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa akizindua upigaji picha za anga  kwa kutumia teknolojia ya ndege ndogo bila rubani (Drone) kwa msaada wa COSTECH katika Kata ya Chapwa, Halmashauri ya Mji wa Tunduma  tarehe 17 Novemba, 2016.

Mkuu wa Mkoa akielezea mpango kabambe wa  upimaji na Urasimishaji ardhi katika Mkoa wa Songwe.    

 Chiku Gallawa alisema kuwa mpango huo ulianzia katika Halmashauri ya Tunduma chini ya MKURABITA  baada ya  kuona ongezeko la Watu ni kubwa na Tunduma ni sehemu ya kuingilia na kutokea   Wageni kutoka nchi za nje.  Aidha aliongeza kuwa upigaji picha  utasaidia kutambua majengo yaliyopo  na kufanya makadirio ya ukusanyaji wa kodi ya majengo kuwa rahisi. Aliongeza kuwa watu waliojenga kwenye vyanzo vya maji, eneo huru la mpaka watajulikana kwa urahisi hivyo kurahisisha namna ya kurekebisha maeneo hayo.  Mwisho aliwashukuru COSTECH kwa mchango wa kitaalam na Teknolojia wanayotumia kupima kwa muda mfupi na gharama ndogo.  

Mkuu wa Mkoa akipata maelezo ya namna ya kuongoza upigaji picha kwa kutumia kompyuta kutoka kwa Wataalam wa COSTECH 


Mkuu wa Mkoa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tundma Mheshimiwa Ally Mwafongo

Ziara ya kukagua shughuli za upimaji  ardhi kwa ajili ya kupanga matumizi ya Ardhi katika Kata ya Kapele, Wilaya ya Momba


Mkuu wa Mkoa akiongoa na Wananchi wa Kijiji cha Kapele umuhimu wa kupanga matumizi ya ardhi. 

Akiongea na wanakijiji hao alisema upangaji wa matumizi ya ardhi ukikamilika matumizi ya ardhi yatakuwa wazi na hakutakuwa na mianya ya rushwa kwa sababu kila kipande cha ardhi kitajulikana matumizi yake.  Aliongeza kuwa ardhi itaongezeka thamani  kwani hati ya kumiliki ardhi inaweza kutumika ili kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za fedha. pia aliwashukuru wanachi kwa ushirikiano wao na Wataalam wa Halmashauri .






 Wanakijiji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa 

Mkuu wa Mkoa akitembelea makazi ya muda ya Wapima Ardhi wa Wilaya ya Momba





Mtaalam Mpima wa ardhi  Kelvin  Tulyanje akimwonesha Mkuu wa Mkoa kazi inavyofyanyika  baada ya kuhamishiwa kwenye Kompyuta 






No comments:

Post a Comment