Saturday, 12 November 2016

SIKU YA UZINDUZI WA UPANDAJI MITI ULIOYOFANYIKA KIMKOA WILAYANI ILEJE


Siku ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa ulifanyika Katika Kijiji cha Ngulilo kilichopo katika kata ya Ngulilo wilayani Ileje tarehe 10 Novemba, 2016


Mkuu wa Mkoa akisamlimiana na Watumishi wa Halmashauri wa Wilaya ya Ileje

Mkuu wa Mkoa akiongea baada ya kusomewa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.         

Akiongoea baada  ya taarifa hiyo Chiku Gallawa alisema uharibifu wa mazingiara unafanya wananchi wasivune sawa na wanavyokeza. alisisitiza kuwa hakuna jinsi nyingine bali ni lazima kuandaa , kusimamia na kutekeleza mikakati ya kurejesha uoto wa asili. aliongeza " hatuhitaji serikali kutuletea misaada kwani tutaonekana tumeshindwa wakati sivyo"

  Mkuu wa Mkoa aliisifu halimashauri ya Ileje kuvuka lengo la kuotesha miche kwani imefikisha miche 1,080,000 wakati lengo la kila Wilaya ni kuotesha miche 1,500,000. 

Pia aliagiza kuwa kati ya miti inayooteshwa inatakiwa kuwa na miche ya miti ya matunda ili baadaye wilaya ziwe na matunda ya kutosha kutegemea  hali ya hewa ya za mazingira husika kwa kuzingatia ushauri wa Wataalam. 

 Pamoja na ushari huo alishangaa kuona kaya zingine zinalima mpaka karibu na kuta za nyumba zao bila kuona mti hata mmoja, hivyo aliagiza kuwa kila kaya ihakikishe inapanda miti karibu na nyumba zao.

UZINDUZI WA KUPANDA MITI KWENYE CHANZO CHA MAJI KILICHOHARIBIWA NA SHUGHULI ZA KILIMO CHA  MSITU WA SERIKALI WA NGULILO




Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akipanda mti kwenye chanzo cha maji cha msitu wa Ngulilo

Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara  Viongozi wa Siasa, Wanafunzi na Wananchi waking'oa mahindi katika eneo la chanjo cha maji cha Ngulilo.






MKUTANO WA KIJIJI BAADA YA KUPANDA MITI











Katika mkutano huo Mkuu wa mkoa alitoa majibu ya maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati, katika hili alianza kwa kuwapongeza Wananchi wa Ileje kwa kuongoza uchangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa asilimia 60 kimkoa. Alishauri kuwa wanaweza kutumia Mkopo wa Bima ya Afya ili kukamilisha uezekaji wa Maboma. 

Aidha,  aliwakumbusha wananchi kuwa Ilani ya Chama Tawala inataka watu wote wajiunge na Mifuko ya Bima za Afya ili kuboresha huduma za Afya nchini. Hivyo alitoa agizo kwa uongozi wa Wilaya kuendelea kuhamasisha wananchi ili waendelee kuchangia na kuhakikisha wanawatambua Wazee wote wasiojiweza na kuwalipia Bima ya Afya.

  Kuhusu hifadhi ya mazingira alisema " Yeyote  anayelima ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji au kando ya mto ajisalimishe na akijisalimisha atapewa adhabu ya kupanda miche ya miti sehemu aliyolima na Mtu ambaye hatajisalimisha sheria itachukua mkondo wake" alisisitiza.

 Akiongelea swala la ufaulu wa Wanafunzi, aliagiza kuwa shule zote zihakikishe zinatoa chakula kwa wanafunzi ili waweze kuwa na afya njema na kufanya vizuri kimasomo. Mkuu wa Mkoa alitoa ushauri kuwa Shule zinaweza kutumia elimu ya kujitemea kulima mashamba ambayo pamoja na kutoa elimu ya kilimo bora watanufaika na chakula kwa ajili ya  Wanafunzi wake. Njia ya pili alisema wazazi wanaweza kuomba kibali cha kuchangisha kwa Mkuu wa Mkoa kupitia kwa Mkuu wa Wilaya au wanaweza kutumia njia zote mbili. 

Mwisho alitakwa wananchi kuongeza moyo wa kujitolea na alizungumzia kuhusu tatizo la barabara na Umeme wa mradi wa REA kutowafikia wananchi kuwa mbali ya njia kuu ya umeme kuwa atavifuatilia.




No comments:

Post a Comment