Na Mwandishi wetu Sia Kisamo - Songwe
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Elias Nawera akiinua DVD juu kama ishara ya kuzindua Filamu ya kikundi cha Fighters Artist Group cha Wilaya ya Songwe tarehe 05 Februari, 2017
Msanii wa Kikindi ... akisoma risala kwa Mkurugenzi wa Wilaya.
Msanii .. alisema lengo la kuandaa filamu hiyo ni kudumisha umoja na mshikamano kati ya wasanii na jamii, kutafuta soko la pamoja
la sanaa, kulinda na kuendeleza utamaduni na pia kushirikiana na taasisi
mbalimbali zitakazokuwa tayari kusaidia uboreshaji wa sanaa kwa lengo la
kujiongezea thamani na kuunganishwa na masoko yenye uhakika
Elias Nawera akipokea nakala ya risala baada ya kusomewa
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya akiongea na Wasanii baada ya uzinduzi
Mkurugenzi wa Wilaya akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Fighter Artist Group
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa filamu inayoitwa "Tamati ya dunia"
Katika hotuba hiyo Elias Nawera aliwahamasisha wasanii kuhakikisha kuwa wanasajiliwa ili kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za
nchi, pia wawe na madhumuni mema ya kutumia sanaa kuelimisha jamii na kujipatia kipato.
Mwisho aliwasihi wasanii kuwa na kazi nyingine za
uzalishaji mali mbali na sanaa kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili
kunufaika na mkopo unaotolewa na halmashauri ya wilaya ya songwe kwa
lengo kuwawezesha vijana kujiongezea kipato.
No comments:
Post a Comment