Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akikagua shamba la mahindi katika kijiji cha Mpui, Momba
Mkuu wa Mkoa alipata muda wa kukagua hali halisi ya mazao
mashambani ambapo alitembelea shamba la
J. Nziku na kuona jinsi mazao yalivyostawi kuonesha hali nzuri ya mvua katika
maeneo hayo.
Akizungumza kuhusu hali ya chakula Chiku Gallawa alisema, Mkoa umejipanga vizuri na uemewaagiza Maafisa
Biashara kutoka maofisini na kuhakikisha wanatafuta masoko ya mazao ya uhakika,
na Maafisa ugani ambao ni Wataalam wa
Kilimo na Maendeleo ya Jamii kuwaelimisha Wakulima mbinu za kilimo bora,
kuongeza thamani mazao na kuwashauri watumiea mavuno yao kwa matumizi sahihi na
siyo kutumia mazao yao kwa kupikia Pombe ambayo kwa uhalisia haina faida zaidi
ya kuleta ugomvi ndani ya familia ambao unamnyima mwanamke haki yake.
Mkuu wa Mkoa akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Mpui wilayani Momba
Mkuu wa Mkoa akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mpui fedha ya kununulia viatu vya shule
Mratibu wa Mradi wa Mkoa wa Songwe Kabambagusha E. akiongea na wanufaika wa fedha za Mfuko wa Jamii (TASAF) katika kijiji cha Mengo , Ndalambo, Momba.
Wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Mpui Momba
Mnufaika wa TASAF Bibi Kasambala akitoa ushuhuda wake jinsi alivyonufaika na fedha za Mfuko wa TASAF. " Mimi nimenunua Kuku, na fedha zingine nimeongezea kununulia bati, sasa nakaa kwenye nyumba iliyoezekwa kwa bati" alieleza Bibi huyo anayeishi katika kijiji cha Kakozi, Ndalmbo, Momba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Momba Adrian Jungu akiongea na wanufaika wa TASAF katika kijiji cha Luasho, Momba
|
Mtaalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa Mwankenja akiongea na Wanufaika wa Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii katika Kijiji cha Luasho, Momba
|
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa atembelea wanufaika wa fedha za TASAF katika wilaya ya Momba.
Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akiwa katika ratiba
yake ya kufuatilia shughuli za maendeleo
ya Wananchi katika ngazi ya vijiji, alitembelea Kijiji cha Mpui ampapo alipata
fursa ya kuongea na Wanufaika wa Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kujua namna wanavyonufaika na fedha hizo
ikiwa ni pamoja na changamoto zake.
Baada ya kuwasikia wanufaika hao, ambao wengi wao walitumia
fedha hizo kwa ajili ya kununulia chakula, kusomeshea watoto, kununua Kuku kwa
ajili ya kufuga na wachache kununulia bati kwa ajili ya kuezekea nyumba, Mkuu
wa mkoa alikuwa na haya ya kusema.
“ Fedha zinazotelewa na Mfuko wa wa TASAF zifanye malengo yaliyokusudiwa”
alisema haya baada ya kusikia kuwa kuna wanafunzi 20 ambao wapo katika orodha
ya wanufaika lakini hawapati huduma stahili kwa sababu walezi wao wanatumia
fedha hizo kwa shughuli zingine,
Mkuu wa mkoa aliagiza
kuwa viongozi wa Serikali ya Kijiji wafuatilie hilo na kuhakikisha kuwa haki
inatendeka kwa watoto ili waendelee na masomo na kupata mahitaji yanayostahili.
Vilevile aliwaagiza Viongozi wa vijjiji kuwafuatilia wazazi
wanaohamia mashamba ya mbali na kuwapa wanafunzi ugumu wa kuhudhuria masomo
wawarejeshe watoto katika maeneo ambayo watahudhuria masomo shuleni kwa urahisi.
Aidha, Chiku Gallawa aliwataka Wataalam na viongozi wa
Vijiji kuona umuhimu wa kuwashirikisha wanufaika wa TASAF katika mpango wa
ruzuku ya pembejeo kwa sababu wana sifa
za kupata ruzuku na itawasaidia kupata uhakika wa chakula.
Ili kufanya ufugaji wa Kuku wenye tija Mkuu wa Mkoa alikemea
ufugaji holela wa kuachia kuku watafute chakula wenye, alisisita ufugaji
unaofuata taratibu za ushauri wa Wataalam na kuzingatia chanjo za mifugo kwa
wakati.
Mkuu wa Mkoa aliendela kutoa agizo kuwa ni maarufuku kukata miti ovyo na kuchoma mkaa kwa sababu hali ya ukataji miti imeharibu mazingira katika maeneo makubwa ya Mkoa na kama tabia hiyo itaendelea Mkoa utatumbukia katika ukame kwa kukosa mvua za kutosha. aliongeza kuwa hata kama mtu amepanda mti wake mwenyewe atatakiwa apate kibali kupitia taratibu sahihi za serikali.
|
No comments:
Post a Comment