Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa katika eneo la kuegesha Malori la Mamlaka ya Mji wa Vwawa, Mbozi, Songwe.
Chiku Gallawa akisikiliza Maswali kutoka kwa Wananchi
Mkuu wa Mkoa akijibu Maswali
Mkuu wa Mkoa wa Sogwe Chiku Gallawa alifanya mkutano wa
hadhara na Wananchi ili kusikiliza kero
zao na kuzitatua katika eneo la kituo cha kuegesha magari ya mizigo Vwawa, Mbozi
Katika kujibu kero za Wananchi alisema,
Kuhusu ardhi alisema, Mkakati wa Mkoa wa Songwe kwanza ni
kukusanya takwimu na kutengeneza rasimu ya mkoa, pili ni urasimishaji ardhi Mjini na Vijijini ili
hata mkulima mdogo mwenye ekari mbili
awe na Hati yake.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi Mwaigomole alisema hati
33,000 zimetolewa kwa kushirikisha wananchi na Afisa Ardhi wa Mbozi Simbeye aliongeza
kuwa ramani ya mipango miji inaendelea kuandaliwa na Wananchi wataendelea
kushirikishwa.
Aidha mkuu wa Mkoa alisema mkoa wa Songwe umepanga kukamilisha
urasimishaji ardhi katika miaka mitatu
hivyo aliwataka Halmashauri ya Mbozi kuazima Wataalam kutoka Halmashauri zingine ndani ya mkoa kusaidiana nao na siyo kungojea mradi
ulete fedha ndiyo kazi ifanyike.
Kuhusu shida ya Maji katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbozi
Mkuu wa Mkoa alisema hilo tatizo linajulikana na ndiyo maana amemwalika Waziri mwenye dhamana ili asaidie kutatua tatizo hilo wakati huu wananchi wajitahidi kuvuna na kutumia maji ya mvua
kwenye mabati ya nyumba.
Vilevile alisema matatizo ya Mama Lishe kwanza yapitie kwa
Mkuu wa Wilaya kabla ya kufika kwake. Na kuingiliana maeneo ya kibiashara
yatatuliwe na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi.
Chiku Gallawa akichambua utata wa eneo ambalo ofisi ya Mkuu wa Mkoa itajengwa ambalo limepelekea gumzo kwa wakazi wa Mamlaka za miji ya Vwawa na Mlowo, alifafanua kuwa, kuna
tofauti ya tafsiri ya Makao makuu ya Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, alisema
Makao Makuu ya Mkoa yamekubaliwa kuwa katika
eneo la Vwawa ambalo litalelewa na Manispaa ambayo itaunganisha Mamlaka
za Miji ya Vwawa na Mlowo na kwamba Makao makuu yahusisha Taasisi mbalimbali na kati ya hizo ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hospitali
ya Mkoa, chuo cha VETA, Magereza,
Polisi, Uhamiaji, na zinginezo. Aliongeza kuwa mpaka sasa maeneo manne
yametambuliwa na yanasubili wataalam wa Mipango Miji na Udongo wapime na kutoa
mapendekezo ya mwonekano wa makao makuu na aina ya majengo kutona na aina ya
udongo.
No comments:
Post a Comment