Balozi Hawa Ndilowe akitoa maelezo ya lengo la ziara yake katika Mkoa wa Songwe.
Maelezo ya Balozi Hawa Ndilowe yalijikita katika kuboresha ushirikiano kati ya wananchi wenye kipato cha chini ambao wamekuwa wakiishi kwa amani na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili za Malawi na Tanzania kwa muda mrefu. Ziara ya Balozi huyo ilibeba vipaumbele katika nyanja za Kilimo, Utalii, Ushirikiano kati ya Wilaya na Wilaya, Mkoa na Mkoa vilevile Maswala ya Ulinzi na Usalama. Aidha, muda mwingi ulitumika kujadili maswala ya Kilimo na Mifugo ambapo baadhi ya maazimio yaliyojitokeza ilikuwa kufikiria namna ya kubadilishana uzoefu wenye mafanikio bora ili kumkwamua mkulima wa kipato cha chini katika upatikanaji wa pembejeo, Uzalishaji na upatikanaji wa Soko sahihi.
Baada ya Maongezi, Walitakiana Kheri katika kudumisha Urafiki, Upendo, Mafanikio ya mwanzo wa safari ya ushirikiano uliowekwa msingi na Balozi wa Malawi Tanzania na Hawa Ndilowe na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa (aliyevaa miwani katika mstari wa mbele) akiwa na Balozi wa Malawi Tanzania Hawa Ndilowe (kushoto kwake) katika picha ya pamoja na Makatibu, Wataalam na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe
|
No comments:
Post a Comment