kikao cha kwanza cha Baraza kamili la Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Songwe kilifanyika tarehe 15 Septemba, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mwambani uliopo Mkwajuni Songwe.
Viongozi iliyosheheni viongozi mbalimbali
Kushoto: Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Godfrey Kawacha na Elias Nawera Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Elias Nawera
Wazee wakaribishwa; wa kwanza kulia, Ismail Isack Nguwingwa mwenyekiti wa mila Tarafa ya Kwimba
Hatimaye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe apatikana.
Na Mwandishi wetu.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Songwe lilimchagua Diwani Abraham Kugaluka kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Halmashauri hiyo. Baada ya kutoa neno la shukrani Mwenyekiti Kagaluka aliitaka TAMISEMI kuwapa motisha watumishi walioshika nafasi za kukaimu ukuu wa Idara wenye sifa zinazostahili wathibitishwe ili waendelee na Idara zao kwa ufanisi zaidi.
Vilevile aliongeza kuwa Serikali ishughulikie stahili za malipo kwa Watumishi kwani kwa kufanya hivyo itapelekea Watumishi kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii hasa katika kipindi hiki cha kuanzisha Wilaya ya Songwe.
Mwenyekiti Kugaluka alimalizia kwa kuwataka Waheshimiwa Madiwani, Watumishi wa Serikali na Wananchi wote wa Songwe kuvunja makundi ya Siasa na kuanza kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi " Hapa kazi tu" alisisitiza.
|
No comments:
Post a Comment