Monday 19 September 2016

KATIBU TAWALA WA MKOA WA SONGWE ELIYA MTINANGI NTANDU AKIONGEA NA WATUMISHI WA SEKRETARIET YA MKOA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Mtinangi Ntandu akiongea na watumishi wa Sekretariet ya Mkoa katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za Makao Makuu ya Mkoa yaliyopo Vwawa, Mbozi tarehe 19 Septemba, 2016. 

Aidha, katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha kwanza kwa Katibu Tawala baada ya kuteuliwa na  Rais  Magufuli. Katibu Tawala alisisitiza kuwa watu waache mazoea ila wafanye kazi kwa ushirikiano katika shida na raha, umakini,  na katika wakati uliopangwa ili kuleta ufanisi wa kazi na kukidhi mahitaji ya watu. 

Katibu Tawala alizungumzia suala la uhaba wa rasilimali na akawaasa Watumishi kutumia rasilimali hizo kwa ushirikiano ili kuleta tija. Vilevile alisisitiza kuwa kila mtumishi atimize wajibu wake kwa umakini ili apate haki yake "Timiza wajibu wako ili upate haki yako" alisisitiza. 

Pia alikemea tabia ya umbea, uongo, majungu na usengenyaji katika maeneo ya ndani na nje ya ofisi. " Tabia hizo ni sumu katika ustawi wa Taasisi yoyote" alikemea

Aliongeza kuwa ni muhimu watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili na kutekeleza maagizo ya Rais "Matokea Makubwa sasa" bila kusukumwa. Hatimaye alisisitiza kuwa Watumishi watapimwa kwa kutumia  mfumo wa OPRAS ambapo aliwataka watumishi wote wajaze fomu hizo kwa wakati.

 



Watumishi wa Sekretariet ya Mkoa wakisikiliza maelekezo ya utendaji kazi kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa.


No comments:

Post a Comment