Monday 31 October 2016

MWANAFUNZI MLEMAVU WA VIUNGO AKABIDHIWA BAISKELI YA KUSUKUMA SEKONDARI YA NALYELYE MBOZI






Afisa Elimu Elimu Maalum Erick Mbunda akitoa akieleza umuhimu wa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa sababu wana uwezo sawa na  wanafunzi wengine. Afisa Elimu alitoa maelezo hayo kwa njia ya kutamka kwa maneno na lugha ya alama



Afisa Elimu, Elimu Maalumu Erick Mbunda akimkabidhi Joshua Haonga Baiskeli ya kusukuma

Joshua Haonga akishukuru baada ya kupewa baiskeli ya kusukuma


Mkuu wa shule ya Sekondari ya Nalyelye Rozi Alberto Mwakyoma akitoa rai kwa wadau mbalimbali alisema "  Kama itawezekana Joshua angehamishiwa kwenye shule ya Bweni kwani mazingira ya shule hii na nyumbani kwa mlezi wake hairidhishi" aliomba


Mwalimu Elizabeth Mwankemwa alisema " Joshua anajitahidi sana katika taaluma na anashirikiana vizuri na wanafunzi "

 Dada mkuu wa shule Esther Mtega alikiri kuwa wanashirikiana vizuri na wenzake pia wanafuzi wote wanampenda Joshua kiasi ambacho wanamchangia anapokuwa amepungukiwa vifaa vya shule kama daftari, Kalamu n.k vilevile wanamsukuma kwenye baiskeli bila kulazimishwa.


Noel Kasebele vilevile alikiri kama Dada Mkuu ila alitoa ombi kwa Serikali na Wadau mbalimbali kuongeza misaada zaidi kwa Joshua

MLEMAVU WA VIUNGO JOSHUA SAMSON HAONGA APATIWA BAISKELI

Na mwandishi wetu.

Joshua ni mwanafunzi ambaye ni  yatima na mlemavu wa viungo, anasoma katika kidatu cha pili katika shule ya Sekondari ya Nalyelye iliyo katika kata ya Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe
Erick Mbunda Afisa  Elimu Elimu Maalum alitoa msaada wa kiti baiskeli ya kusukumwa baada ya kuona matatizo aliyokuwa akiyapata mwanafunzi huyo kupitia kwa Waalimu.
Aidha Mbunda alisema kuwa aliomba msaada wa baiskeli hiyo kutoka kwa msamalia mwema anayeishi Njombe ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Afisa huyo alisema kuwa amekuwa akisaidia wanafunzi wenye ulemamvu na wasio wanafunzi bila kujali umri wao. Vilevile aliwashukuru wanafunzi na Waalimu kwa moyo wao wa kumsaidia Joshua wakati akitumia baiskeli iliyokuwa inaharibika mara kwa mara.

Mwalimu Mkuu Roze Alberto Mwakyoma alisema, pamoja na misaada inayotolewa kutoka kwa Waalimu, Wanafunzi na Mdau huyo, alitoa  rai kuwa Joshua angeweza kufanya vizuri kama angepata shule ya wenye uhitaji kama Yeye au Shule ya Bweni kwa  sababu mvua zikinyesha anashindwa kufika shuleni pia mazingira ya nyumbani kwa mlezi wake hayawezi kufanana na bweni.

Mlezi wa Joshua alikiri kuwa hana uwezo wa kumlea Joshua inavyotakiwa, alisema “ mimi nina watoto wengi na maisha yangu na mke wangu ni biashara ndogo na kilimo wakata Joshua anakiwa kuwa na mtu jirani kwani hawezi kujihudumia kwa lolote, pia choo change  sababu ana watoto wengi na maisha yao yanategemea kilimo na biashara ndogo wakati huo Joshua hawezi kujitegemea kwa lolote hata kwenda chooni hawezi kwenda mwenyewe. Naomba serikali inisaidie inisaidie” alisisitiza.




Bustani ya Shule ya Nalyelye yenye miche 2400 katika kutekeleza agizo la Mkoa la kuotesha miche ya miti 2000 kwa kila Shule


No comments:

Post a Comment