Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akikabidhiwa mabati 1,200 kutoka kwa Maneja wa Kampuni ya PRNG Mineral Limited Patrick Ochieng tarehe 05 Oktoba, 2016 nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyopo Vwawa, Mbozi.
Kampuni ya PRNG ipo katika mchakato wa kupata leseni ili ianze kuchimba rasmi madini ya sumaku yenye uwiano wa kipekee wa madini ya neodymium na praeseodymium.
Vilevile katika eneo la kaskazini ya Ngualla kuna madini aina ya niobium - tantalium na phosphate.
Mkuu wa Mkoa akitoa shukrani kwa Kampuni ya PRNG Mineral Limited.
Katika shukrani hizo Mkuu wa Mkoa alisema misaada inayotolewa na wadau hupokelewa katika mfumo wa serikali na kusambazwa kwenye miradi ambayo wananchi wametoa michango yao ya ujenzi wa maboma hadi kufikia hatua ya kuezeka. Aidha alisema mpaka kipindi hiki Mkoa una upungufu wa mabati yasiyopungua 150, 000. Hatimaye alitoa wito kwa wadau mbalimbali kupenda kutoa michango ya aina mbalimbali ili kuifikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda mwaka 2025
Mkuu wa Mkoa Chiiku Gallawa akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa, Wawakilishi wa Kampuni ya PRNG Minerals Limited na Wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa
|
No comments:
Post a Comment