|
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akifanya mkutano katika a Kijiji cha Chipumpu. tarehe 05/10/2016
|
|
Mkuu wa Mkoa akifafanua umuhimu wa kuacha kilimo cha mazoea na kuanza kilimo biashara.
|
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa alifanya ziara katika vijiji vya Chipumpu, Kapele na Kasinde ambavyo vipo katika kata
ya kapele Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe tarehe 05 Oktoba, 2016. Mkuu wa mkoa aliongozana na kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe na wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa na
Wataalamu wa Wilaya ya Momba.
Katika ziara hii Mkuu wa Mkoa
alihamasisha suala la maendeleo katika vijiji hivyo na kueleza dhamira ya
Serikali kutoka katika kipato cha chini kwenda katika kipato cha kati. Vilevile
kuipeleka Tanzania katika nchi ya Viwanda ifikapo 2025.
Aidha, Chiku Gallawa alitumia muda huo
kujiridhisha kwa Wananchi kama mihtasari iliyo wasilishwa na Mwekezaji Nkusu
Theo Sugar Limited ilikuwa ni ridhaa ya pande zote mbili kati ya Mwekezaji na
Wananchi.
|
Mkutano katika kijiji cha Kapele
Mkuu wa Mkoa akitoa ufafanuzi kwa wananchi umuhimu wa kutunza mazingira. kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Juma Irandu na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mwaijulu J.D
Mkuu
wa Mkoa alikemea ukataji wa miti kiholela unaoendelea katika kijiji.
Hivyo kukemea wahamiaji wakifugaji wanaohamia bila kufata taratibu na viongozi
wanao wakaribisha bila kufuata utaratibu. Alisisitiza kuwa kila mhamiaji
atakayetaka kuhamia hapo kijijini ajadiliwe kwenye mkutano Mkuu wa Kijiji na wanayo mamlaka ya kumkubali na kumkataa.
Mkutano katika kijiji cha Kasinde
Mkuu wa Mkoa akisisitiza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kukifanya Kijiji cha Kasinde kuwa kijiji cha Biashara.
|
Mkuu wa Mkoa aliwaeleza
wananchi kwamba, Serikali imedhamiria kuhama kutoka uchumi wa chini mpaka
uchumi wa kati kwa kuhakikisha kipato cha mtu mmoja mmoja kinakua. Watu wawe na
kipato kuanzia milioni 6 mpaka milioni 20. Alisema “ sasa tunaanza na
urasimishaji wa ardhi ili kila mwananchi awe na hati ya eneo lake. Hivyo
hatutakiwi kuanza kuuza ardhi yetu kwa sasa. Kwa kuwa kwa ekari moja mnavuna
gunia 15 za mpunga, inabidi mvune gunia 45 kwa ekari moja. Yatupasa kukifanya
kijiji cha Kasinde kiwe kijiji biashara”. Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wananchi kuwa Mkoa
umeanza kukusanya takwimu kwa ajili ya
kupanga maendeleo ya kimkoa. Pia aliongeza kuwa kijiji kianze kusimamia katika
kutunza mazingira. Aliagiza kuwa “tuache
kukata miti ovyo, Pia tuache kukaribisha wageni bila kufuata utaratibu ili
kuzuia migogoro isiyo ya lazima”. alisisitiza
No comments:
Post a Comment