Wednesday, 28 September 2016

BALOZI WA MALAWI TANZANIA HAWA NDILOWE ATEMBELEA MKOA WA SONGWE

Balozi wa Malawi nchini Tanzania Hawa Ndilowe akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa  katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa zilizopo Vwawa, Mbozi, Songwe tarehe 28 Septemba, 2016.


Balozi Hawa Ndilowe akiandika katika kitabu cha Wageni Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa.


Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akitoa taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa  Balozi Hawa Ndilowe


Balozi Hawa Ndilowe akitoa maelezo ya lengo la ziara yake katika Mkoa wa Songwe. 

 Maelezo ya Balozi Hawa Ndilowe yalijikita katika kuboresha ushirikiano kati ya wananchi  wenye kipato cha chini  ambao wamekuwa wakiishi kwa amani na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili za Malawi na Tanzania kwa muda mrefu.  Ziara ya Balozi huyo ilibeba vipaumbele katika nyanja za Kilimo, Utalii, Ushirikiano kati ya Wilaya na Wilaya, Mkoa na Mkoa vilevile Maswala ya Ulinzi na Usalama.  Aidha, muda mwingi ulitumika kujadili maswala ya Kilimo na Mifugo ambapo baadhi ya maazimio yaliyojitokeza ilikuwa kufikiria namna ya kubadilishana uzoefu wenye mafanikio bora ili kumkwamua mkulima wa kipato cha chini katika upatikanaji wa pembejeo, Uzalishaji na upatikanaji wa Soko sahihi.


Baada ya Maongezi, Walitakiana Kheri katika kudumisha Urafiki, Upendo, Mafanikio ya mwanzo wa safari ya ushirikiano uliowekwa msingi na Balozi wa Malawi Tanzania na Hawa Ndilowe na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa (aliyevaa miwani katika mstari wa mbele) akiwa na Balozi wa Malawi Tanzania Hawa Ndilowe  (kushoto kwake) katika picha ya pamoja na  Makatibu, Wataalam na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe

MPANGO WA JUMLA WA MJI WA TUNDUMA 2015 - 2025

Timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma ikiwasilisha Mpango wa Jumla wa Mji wa Tunduma  kwa kipindi cha 2015 - 2026 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa na Wataalam wake kwenye ukumbi wa mkuu wa Mkoa Vwawa tarehe 26 Septemba, 2016.

Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa na Wataalam wake wakisikiliza uwasilishaji wa mpango huo kutoka kwa Afisa Mipango Miji wa Tunduma Mutta D.P.B


Wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Mji wa Tunduma wakisikiliza  Maada hiyo.

 


Monday, 19 September 2016

BARAZA KAMILI LA MADIWANI SONGWE

kikao cha kwanza cha Baraza kamili la Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Songwe kilifanyika tarehe 15 Septemba, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mwambani  uliopo Mkwajuni Songwe.


Viongozi iliyosheheni viongozi mbalimbali 



Kushoto: Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Godfrey Kawacha na Elias Nawera Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe.




Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Elias Nawera



Wazee wakaribishwa; wa kwanza kulia, Ismail Isack Nguwingwa mwenyekiti wa mila Tarafa ya Kwimba


Hatimaye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe  apatikana.

Na Mwandishi wetu.

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Songwe lilimchagua  Diwani Abraham Kugaluka kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Halmashauri hiyo. Baada  ya kutoa neno la  shukrani Mwenyekiti Kagaluka aliitaka TAMISEMI kuwapa motisha watumishi walioshika nafasi za kukaimu ukuu wa Idara wenye sifa zinazostahili wathibitishwe ili waendelee na Idara zao kwa ufanisi zaidi.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali ishughulikie stahili za malipo kwa Watumishi kwani kwa kufanya hivyo itapelekea Watumishi kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii  hasa katika kipindi hiki cha kuanzisha Wilaya ya Songwe.

 Mwenyekiti Kugaluka alimalizia kwa kuwataka Waheshimiwa Madiwani, Watumishi wa Serikali na Wananchi wote wa Songwe kuvunja makundi ya Siasa na kuanza kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi " Hapa kazi tu" alisisitiza.


KATIBU TAWALA WA MKOA WA SONGWE ELIYA MTINANGI NTANDU AKIONGEA NA WATUMISHI WA SEKRETARIET YA MKOA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Mtinangi Ntandu akiongea na watumishi wa Sekretariet ya Mkoa katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za Makao Makuu ya Mkoa yaliyopo Vwawa, Mbozi tarehe 19 Septemba, 2016. 

Aidha, katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha kwanza kwa Katibu Tawala baada ya kuteuliwa na  Rais  Magufuli. Katibu Tawala alisisitiza kuwa watu waache mazoea ila wafanye kazi kwa ushirikiano katika shida na raha, umakini,  na katika wakati uliopangwa ili kuleta ufanisi wa kazi na kukidhi mahitaji ya watu. 

Katibu Tawala alizungumzia suala la uhaba wa rasilimali na akawaasa Watumishi kutumia rasilimali hizo kwa ushirikiano ili kuleta tija. Vilevile alisisitiza kuwa kila mtumishi atimize wajibu wake kwa umakini ili apate haki yake "Timiza wajibu wako ili upate haki yako" alisisitiza. 

Pia alikemea tabia ya umbea, uongo, majungu na usengenyaji katika maeneo ya ndani na nje ya ofisi. " Tabia hizo ni sumu katika ustawi wa Taasisi yoyote" alikemea

Aliongeza kuwa ni muhimu watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili na kutekeleza maagizo ya Rais "Matokea Makubwa sasa" bila kusukumwa. Hatimaye alisisitiza kuwa Watumishi watapimwa kwa kutumia  mfumo wa OPRAS ambapo aliwataka watumishi wote wajaze fomu hizo kwa wakati.

 



Watumishi wa Sekretariet ya Mkoa wakisikiliza maelekezo ya utendaji kazi kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa.


Sunday, 18 September 2016

BRN - STAR RATING ASSESSMENT REPORT IN SONGWE REGION


Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Godfrey Kawacha akipokea ripoti ya utafiti wa Matokeao Makuu Sasa katika sekta ya Afya kutoka kwa Mtafiti Dr. Aloyce F. Lengesia  kwenye ukumbi wa mkuu wa Mkoa Vwawa, Mbozi Songwe tarehe 09 Septemba, 2016

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dr. Lazaro akipokea nakala ya taarifa ya utafiti huo kutoka wa Dr.  Aloyce F. Lengesia
Dr. Lengesia akiwasilisha matokea ya utafiti kwa Sekretariet ya Mkoa wa Songwe

Friday, 9 September 2016

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa apokea mabati kutoka kampuni ya Machimbo ya Dhahabu ya Shanta

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea mchango wa mabati 2,400 kutoka kwa Meneja wa Mgodi  wa machimbo ya dhahabu Scott Yelland yalipo katika wilaya ya Songwe.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika eneo la Ofisi za Mkuu wa Mkoa lililopo katika Vwawa, Mbozi tarehe  08 Septemba, 2016.



Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe,  Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi  na Waandishi wa Habari wakiwa katika sherehe ya kukabidhian mabati.


Sunday, 4 September 2016

SIKU YA KUPATWA KWA JUA RUJEWA MBARALI TAREHE 01 SEPTEMBA, 2016




     Mtaalam wa elimu ya anga akiwafundisha watalii wa ndani namna ya kutumia darubini






Makundi yote yalishirki kuangalia kupatwa kwa Jua


Mkuu wa Mkoa akiangalia hatua za kupatwa kwa Jua

Add caption

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa kwenye kiwanda cha Karatasi cha Mufindi Iringa tarehe 01Semptemba,2016





Msimamizi mkuu wa shughuli  za maabara ya kiwanda akitoa ujumbe wake kwa wanawake

Picha ya mwisho ya pamoja baada ya kuangalia hatua mbalimbali za utengenezaji wa karatasi 

kiwandani

Mkuu wa Mkoa akipata maelezo ya upimaji wa uimara wa karatasi kutoka kwa Mtaalam wa Maabara ya Kiwanda Beatrice Kigoda


Mkuu wa Mkoa akijadiliana na Mtaalam wa Maabara Beatrice kuhusu utendani wa Kiwanda


Add caption

Mkuu wa Mkoa na timu yake wakishuka ngazi kutoka sehemu ya juu ya mtambo wa kukata magogo ya miti katika vipande vidogo .

Mtaalam wa Maabara Beatrice Kigoda akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa na timu yake kwenye maeneo mbalimbali ya Kiwanda

Mkuu wa Mkoa na timu yake ya wataalam wakielekea maeneo mbali mbali  ya Kiwanda.

Mkuu wa Mkoa akioneshwa aina mbalimbali za karatasi zinazotengenezwa na Kiwanda

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipata maelezo ya Kiwanda kutoka kwa Mtaalam wa Maabara Beatrice Kigoda