Tuesday, 25 October 2016

KATIBU TAWALA WA MKOA WA SONGWE AKABIDHIWA MADAWATI 400 NA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU NYANDA ZA JUU KUSINI

Sherehe ya kukabidhi Madawati kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) zilizofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Mkuu wa Mkoa Songwe   tarehe 25 Oktoba, 2016.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda Nyanda za juu Kusini Denis Kweslema akitoa taarifa  kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya M. Ntandu kuhusu mchango wa Madawati.

Katibu Tawala wa Mkoa akikata utepe kama ishara ya kuzindua sherehe ya kukabidhiwa madawati


Katibu Tawala wa Mkoa akipeana mikono na Kamu Meneja wa TFS baada ya kukabidhiwa madawati 400

Katibu Tawala akitoa neno la shukrani kwa mchango aliokabidhiwa kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu na Wadau mbalimbali. katika shukrani zake alisema " Madawati haya tutayasambaza kwa kuzingatia mahitaji" aliongeza kwa kutoa wito kwa wadau wengine kutoa michango kwa sababu bado kuna mahitaji ya madawati, Mabati na Saruji katika huduma za Elimu na Afya Mkoani Songwe.

Picha ya pamoja ya Katibu Tawala, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi wa Wilaya na Timu ya Huduma za Misitu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Picha ya pamoja ya Katibu Tawala, Timu ya Huduma za Misitu, Wataalam Ofisi ya Sekretarieti ya Mkoa na Wakurugenzi wa Wilaya za Mkoa wa Songwe.

KIKAO KAZI CHA KAMATI ZA MITIHINANI ZA HALMASHAURI ZA WILAYA MKOA WA SONGWE

Kikao cha kazi  cha Kamati Za Mitihani  Mkoa wa Songwe kuhusu Maandalizi, Mapokezi, Ugawaji na Usimamizi wa mitihani  ya kidato cha nne kilichofanyika tarehe 25 Oktoba, 2016 kwenye Ukumbi wa  Halmashauri ya  Wilaya ya Mbozi,  Songwe. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya M. Ntandu akitoa maelekezo kwa wanasemina. Katibu Tawala aliwasisitiza washiriki wa kikao umuhimu wa Uadilifu, Uaminifu, Ushirikiano katika zoezi zima la Mitihani.







Washiriki wakisikiliza kwa umakini


Sunday, 23 October 2016

CHIFU WA KABILA LA WABUNGU KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO MKWAJUNI

Chifu wa Kabila la Wabungu Chifu Mwamvongo (aliyeshika finbo, kavaa kofia ya kijani na njano) akiwa na Wazee wa Mila kabla ya kuanza kikao cha kutatua mgogoro wa mahali pa kuzika Machifu.

Chifu Mwavongo akitoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa eneo la kufanyia mazishi la Amaponga kuwa lipo katika Kata ya Mwambani na  eneo hilo limekuwa likitumika tangu miaka 130 iliyopita. Kikao hicho kiliamua kuwa eneo hilo litatumika kwa ajili ya kuzikia Machifu tu. kikao hicho kilimkaribisha Afisa utamaduni , Michezo na Vijana wa Wilaya ya Songwe Sia Kisamo ( mwenye gauni lenye rangi ya njano na weusi) tarehe 21 Oktoba, 2016.


SIKU YA USAFI MKWAJUNI, SONGWE



Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah (Aliyevaa shati la Kitenge na Kofia nyeupe) akiongoza Wataalam na  wananchi katika zoezi la usafi wa Mazingira Mkwajuni, Songwe tarehe 22 Oktoba, 2016



Tuesday, 11 October 2016

ZIARA YA MKUU WA MKOA CHIKU GALLAWA KATIKA KATA YA KAPELE








Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa  akifanya mkutano katika a Kijiji cha Chipumpu.  tarehe 05/10/2016

Mkuu wa Mkoa akifafanua umuhimu wa kuacha kilimo cha mazoea na kuanza kilimo biashara.


 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa alifanya ziara katika vijiji vya Chipumpu, Kapele na Kasinde ambavyo vipo katika kata ya kapele Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe tarehe 05 Oktoba, 2016. Mkuu wa mkoa aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe na wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa na Wataalamu wa Wilaya ya Momba.
Katika ziara hii Mkuu wa Mkoa alihamasisha suala la maendeleo katika vijiji hivyo na kueleza dhamira ya Serikali kutoka katika kipato cha chini kwenda katika kipato cha kati. Vilevile kuipeleka Tanzania katika nchi ya Viwanda ifikapo 2025.
 Aidha, Chiku Gallawa alitumia muda huo kujiridhisha kwa Wananchi kama mihtasari iliyo wasilishwa na Mwekezaji Nkusu Theo Sugar Limited ilikuwa ni ridhaa ya pande zote mbili kati ya Mwekezaji na Wananchi.

Mkutano katika kijiji cha Kapele

Mkuu wa Mkoa akitoa ufafanuzi kwa wananchi umuhimu wa kutunza mazingira. kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Juma Irandu na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mwaijulu J.D

Mkuu wa Mkoa alikemea ukataji wa miti kiholela unaoendelea katika kijiji. Hivyo kukemea wahamiaji wakifugaji wanaohamia bila kufata taratibu na viongozi wanao wakaribisha bila kufuata utaratibu. Alisisitiza kuwa kila mhamiaji atakayetaka kuhamia hapo kijijini ajadiliwe kwenye  mkutano Mkuu wa Kijiji  na wanayo mamlaka ya kumkubali na kumkataa.

Mkutano katika kijiji cha Kasinde


 Mkuu wa Mkoa akisisitiza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kukifanya Kijiji cha Kasinde kuwa kijiji cha Biashara.


Mkuu wa Mkoa aliwaeleza wananchi kwamba, Serikali imedhamiria kuhama kutoka uchumi wa chini mpaka uchumi wa kati kwa kuhakikisha kipato cha mtu mmoja mmoja kinakua. Watu wawe na kipato kuanzia milioni 6 mpaka milioni 20. Alisema “ sasa tunaanza na urasimishaji wa ardhi ili kila mwananchi awe na hati ya eneo lake. Hivyo hatutakiwi kuanza kuuza ardhi yetu kwa sasa. Kwa kuwa kwa ekari moja mnavuna gunia 15 za mpunga, inabidi mvune gunia 45 kwa ekari moja. Yatupasa kukifanya kijiji cha Kasinde kiwe kijiji biashara”.  Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wananchi kuwa Mkoa umeanza kukusanya takwimu  kwa ajili ya kupanga maendeleo ya kimkoa. Pia aliongeza kuwa kijiji kianze kusimamia katika kutunza mazingira. Aliagiza kuwa  “tuache kukata miti ovyo, Pia tuache kukaribisha wageni bila kufuata utaratibu ili kuzuia migogoro isiyo ya lazima”. alisisitiza

Friday, 7 October 2016

MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA AKABIDHIWA MABATI NA KAMPUNI YA PRNG MINERAL LIMITED

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akikabidhiwa mabati  1,200  kutoka kwa  Maneja wa Kampuni  ya  PRNG Mineral Limited Patrick Ochieng  tarehe 05 Oktoba, 2016 nje ya ofisi ya Mkuu  wa Mkoa iliyopo Vwawa, Mbozi.

Kampuni ya PRNG ipo katika mchakato wa kupata leseni ili ianze kuchimba rasmi madini ya sumaku yenye uwiano wa kipekee wa madini ya neodymium na praeseodymium.

Vilevile  katika eneo la kaskazini ya Ngualla kuna madini aina ya niobium - tantalium na phosphate. 

Mkuu wa Mkoa akitoa shukrani kwa Kampuni ya PRNG Mineral Limited.

 Katika shukrani hizo Mkuu wa Mkoa alisema misaada inayotolewa na wadau hupokelewa  katika mfumo wa serikali na kusambazwa kwenye miradi ambayo wananchi wametoa michango yao ya ujenzi wa maboma hadi kufikia hatua ya  kuezeka. Aidha alisema mpaka kipindi hiki Mkoa una upungufu wa mabati yasiyopungua 150, 000. Hatimaye alitoa wito kwa wadau mbalimbali kupenda kutoa michango ya aina mbalimbali  ili kuifikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda mwaka 2025


Mkuu wa Mkoa Chiiku Gallawa akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa

Tuesday, 4 October 2016

MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA AKUTANA NA WADAU WA ELIMU KATIKA WILAYA YA MBOZI

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameongea na Wadau wa Elimu katika Wilaya ya Mbozi tarehe 04 Oktoba, 2016 katika ukumbi shule ya Sekondari ya Vwawa iliyopo Mbozi, Songwe


Mkuu wa Mkoa akiongea na Wadau wa Elimu