Tuesday, 28 February 2017

TAASISI YA KIFEDHA YA BAYPORT YATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGWE

Meneja wa  Taasisi ya fedha ya Bayport kanda za juu kusini  Emmanuel Nzutu (aliyevaa shati jeupe wa nne kutoka kulia ) akimkabidhi Kompyuta  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe  Wakili Elias Nawera.


BAYPORT WATOA KOMPYUTA MBILI KWA AJILI YA MATUMIZI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGWE

Na Sia Kisamo -  Afisa Utamaduni Songwe

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe na kuhudhuriwa na baadhi ya Wataalam, Meneja wa Taasisi hiyo alisema kuwa, wanathamini utendaji wa Halmashauri kwa maendeleo ya wananchi ndiyo maana wameamua kutoa msaada wa Kompyuta mbili za mezani  ili  kurasisha utekeleza wake.
Naye Mkurugenzi wa Wilaya alitoa shukrani na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika nyanja mbalimbali ili kutimiza adhma ya serikali kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Sunday, 19 February 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ileje akutana na Machifu wa Ileje


Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude akiwa na baadhi ya machifu wa wilaya hiyo baada ya kufanya nao kikao katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya Ileje. mh Joseph Mkude akiwa na chifu wa kabila la Walambya lililopo wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya akiwa na Chifu wa Kabila la Walambya

Chifu wa Walambya Sisimbe Shalala Mwampashi kutoka kijiji cha Mlale Wilayani Ileje

KIKAO CHA MKOA CHA WADAU WA ELIMU ILI KUJITATHMINI NA KUPANGA MIKAKATI YA KUINUA ELIMU KATIKA MKOA WA SONGWE


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akifungua kikao cha Wadau wa Elimu Mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa sekondari ya Vwawa tarehe 13 February, 2017.



Mwenyekiti wa kikao hicho Mh.Eliya Ntandu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ileje (kulia) wakipitia mambo kadhaa yaliyojadiliwa katika kikao hicho



Pistory Mashiku mdau wa elimu kutoka Ileje akisoma maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.


Wadau wa Elimu toka wilya ya Ileje wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe.



Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje Haji Mnasi akitoa taarifa ya Halmashauri yake.




WADAU WA ELIMU WAJITWISHA JUKUMU LA KUUKWAMUA MKOA WA SONGWE KITAALUMA
Na:Daniel Mwambene,Songwe
Katika kuukwamua mkoa wa Songwe kwenye aibu ya kushika nafasi ya mwisho tena kitaifa katika matokeo yajayo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2017 na kuinua kiwango cha Elimu ya Sekondari wadau wamegawana majukumu na kuahidi kushika nafasi za juu kitaifa.
Mkakati huo ulifikiwa kwenye kikao cha Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Songwe kilichofanyika katika ukumbi wa sekondari ya Vwawa kikiongozwa na viongozi wa mkoa huo ukihusisha Wakuu wa Wilaya,Makatibu Tawala,Wakurugenzi Watendaji Maafisa Elimu, baadhi Maafisa Elimu Kata,walimu wa sekondari na Asasi zisizo za kiserikali.
Wadau wengine ni walimu ambao shule zao zilifanya vizuri na zilizofanya vibaya na kusababisha mkoa kuwa wa mwisho kutoka  halmashauri zote tano za mkoa huo ambazo ni Songwe,Momba, Ileje,Mbozi, na Tunduma Mji.
Akifungua kikao hicho,Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gallawa aliwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kuacha mtindo wa kukaa ofisini badala yake wawafuate wananchi katika maeneo yao hali itakayowapunguzia wananchi gharama za kuwafuata viongozi ambao serikali imewapatia vyombo vya usafiri.
Alisema kuwa,viongozi wa serikali hawana budi kujenga utamaduni wa kuwatumikia wananchi ili kupokea kero zao pamoja na kujionea hali halisi kuliko kusubiri taarifa za mezani.
Mh.Gallawa aliongeza,kuwa kiongozi yeyote atakayeonekana kuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi kamwe serikali ya mkoa wake haitamvumilia.
Baadhi ya mikakati iliyowekwa ni pamoja na taarifa za Wathibiti Ubora wa Elimu kufanyiwa kazi na kila mlengwa,uboreshaji wa mazingira ya shule,upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni,jamii kuelimishwa ili kuondokana na imani za kishirikina kujenga nidhamu kwa wanafunzi,kuthibiti utoro wa walimu na wanafunzi.
Mambo mengine ni kutafuta walimu wa mbadala kwenye masomo yasiyo na walimu,mgawanyo mzuri wa walimu na kutumia njia shirikishi na fikirishi katika kujifunza na utoaji wa motisha chanya kwa wanafunzi na wadau wa elimu mkoani humo watakaofanya vizuri.
Ikumbukwe kuwa mkoa huo wenye umri wa miezi takribani kumi tangu kuanzishwa kwake katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mkoa huo ulishika nafasi ya mwisho kwa mikoa yote ya Tanzania Bara.
Kabla ya kufikia hatua ya kupanga mikakati hiyo kila halmashauri ilitoa taarifa yake iliyotokana na vikao vya wadau kutoka ngazi za wilaya ambayo pia ilitokana na mikakati ya ngazi za kata ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo aliyoyatoa mwishoni mwa mwaka jana wakati wa kutolewa kwa matokeo ya Darasa la Saba 2016.
Akifunga kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa huo  Eliya Ntandu alizitaka halmashauri zote kwenda kutekeleza maazimio hayo kwa kuwa na mpango kazi unaotekelezeka na kupimika.

Ntandu alisema kuwa kila mkakati uliopangwa utafuatiliwa na kila kiongozi kwenye eneo husika la utekelezaji na atakayelelega hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.