Monday, 29 August 2016
Sunday, 28 August 2016
KIKAO CHA KAZI NA WATAALAM MKOA WA SONGWE TAREHE 26 AGOSTI,2016
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akimkabidhi Ipad Afisa TEHEMA wa wilaya ya Momba Alfred Simpoli baada ya kikao cha kazi kilichohusu namna ya kuwakomboa vijana kiuchumi katika Mkoa wa Songwe. |
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akimkabidhi Ipad Afisa Utamaduni wa wilaya ya Songwe Sia baada ya kikao cha kazi.
SIKU YA USAFI MKOA WA SONGWE TUNDUMA TAREHE 27 AGOSTI, 2016
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Songwe akifanya usafi katika eneo la Kilimanjaro Tunduma tarehe 28 Agosti, 2016 |
![]() |
Wananchi wakitanya usafi katika eneo la kata ya Majengo |
![]() |
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishirikiana na wananchi kufanya usafi katika eneo la Kituo cha Mabasi kikuu kilichopo katika kata ya Majengo |
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Modest Mkude (mwenye kofia) akiongea na wanachi baada ya kufanya usafi katika eneo la gulio la Iboya lililopo katika kata ya Majengo |
![]() |
Afisa Tarafa ya Tunuduma Edward Lugongo akiongea na Wananchi |
![]() |
Shughuli za usafi zikiendelea katika eneo la kata ya Tunduma |
![]() |
Mkuu wa Mkoa akipata maelekezo ya usafi wa mji wa Tunduma kutoka kwa Mtendaji wa Kata ya Tunduma Mohamed Kaguo |
Siku ya usafi katika Mkoa wa Songwe iliyanyika Tunduma tarehe 27 Agosti,2016
Akizungumza na wananchi wa eneo la Kisimani
![]() |
Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa kwa umakini |
Thursday, 25 August 2016
ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SONGWE KATIKA WILAYA YA MOMBA
Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akivuka daraja la kuning'inia kutoka Kamsamba wilaya ya Momba kwenda Kilyamatundu wilaya ya Sumbawanga
ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA TAREHE 22 - 23 AGOSTI, 2016
Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akivuka mto Momba baada ya kutembelea kijiji cha Kilyamatundu kilichopo katika Wilaya ya Sumbawanga
ZIARA YA MKUU WA MKOA KATIKA WILAYA YA MOMBA
Friday, 5 August 2016
ZIARA YA WAZIRI WA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MHE. GEORGE SIMBACHAWENE (MBUNGE) KATIKA MKOA WA SONGWE.
Waziri George Simbachawene na Mkuu wa Mkoa wakielekea Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuongea na Watumishi.
Waziri akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Aloyce Tuwoneye Mdalavuma
Ziara ya Waziri wa Ujennzi, Uchukuzi na Mawasilano Prof. Makame Mbalawa Mkoani Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbalawa amesema hakubaliani na hali ya ujenzi wa jengo la
kupokelea wageni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Songwe na hivyo kuahidi
kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na thamani halisi ya fedha iliyotumika na
taratibu za kumpata mkandarasi aliyejenga.
Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi ya
Mkuu wa mkoa wa Songwe alipofanya ziara ya siku moja kuwa hajaridhika na hali
ya jingo lilivyo licha ya serikali kutoa fedha nyingi huku jingo hilo likiwa
halijakamilika na mkandarasi hayupo katika eneo la kazi kwa muda mrefu.
Alisema miundombunu ya ujenzi wa
majengo katika uwanja huo hakubaliani nayo wakati uwanja ukiwa umejengwa vizuri
na kuwa serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ujenzi unakamilika na ndege
kubwa zikiwemo za mizigo zianze kutua ili kusaidia kusafirisha mizigo ya
wakulima na hivyo kuinua uchumi wao.
“Tumejenga vizuri barabara ya kurukia
ndege lakini tunashangaa hatua ua jingo hilo hairidhishi na siko tayari
kulipokea hadi hapo nitakapojiridhisha” alisema Mbalawa
Alisema kufuatia hali hiyo serikali
itaunda timu ya kufuatilia namna mkandarasi huyo alivyopatikana, thamani halisi
ya fedha ikijiridhisha ndipo itakapotoa fedha za kumalizia ujenzi huo ili
huduma ziendelee.
Waziri huyo alisema kwa kuzingatia
umuhimu wa miundombinu ya mawasiliano sasa serikali ya awamu ya tano imeamua
kuwasaidia wananchi ambao wanapata shida kwa kutenga asilimia 46 ya bajeti ya
mwaka 2016 hadi 2017 ambayo ni sawa ni zaidi ya Sh. 1.2 tilioni zikiwa
zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu.
Kwa upande wake meneja wa uwanja wa
Songwe Hamisi Amiri alisema mkandarasi wa kwanza ambaye ni kampuni ya
Kundasighn aliacha kuendelea na ujenzi hali ambayo imesababisha kutokukamilika
kwa wakati.
Alisema kwa sasa kuna kampuni nyingine
ya Shamphrey ambao wameanza kujenga miundombinu ya majengo ambapo hadi sasa
mkandarasi huyo hajalipwa kiasi chochote cha pesa hali inayosababisha kzi ya
ujenzi kuendelea kusuasua.
Stephano Simbeye, Mwananchi
simbeyesjmwananchi@gmail.com
Watumishi ngazi ya Mkoa na Halmashauri wakimsikiliza Waziri.
Watumishi ngazi ya Mkoa na Halmashauri wakimsikiliza Waziri.
Ziara ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Mkoani Songwe
Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya pembejeo kwa Waziri.
Hali ya afya ya udogo katika mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini inadaiwa kuzidiwa na tindikali nyingi, hivyo kuwa chanzo
cha kushuka kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali na hivyo kuwakosesha tija
wakulima.
Hayo yameelezwa jana na wadau na
watafiti katika shamba la Mbegu la Mbozi lililopo eneo la Magamba mkoani Songwe
kwa Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi Dkt. Charles Tizeba kuwa hali ya udongo
imekuwa kikwazo kutokana na kuwa licha ya kutumia mbolea za chumvi chumvi
lakini hazitoi matokeo mazuri kwa mkulima.
Robert Hamisi ni mtaalamu wa uzalishaji
mbegu kutoka Kampuni ya Meru alisema kuwa katika eneo la hekta 220, uzalishaji
ulikuwa tani 2.5 hali iliyofanya washituke na kuomba ushauri kwa Kampuni ya
Yara ambao walifika shambani hapo na kuchukua sampuli ya udongo na kwenda
kupima maabara nchini Norway.
Alisema baada ya kupata majibu ya kipimo
cha udongo walishauriwa aina ya mbolea ya kutumia ili kurejesha afya ya udungo
inayoongeza virutubisho vilivyopotea na sasa mwaka huu mavuno yameongezeka na
kwamba wamelipa hekta 310 wanatarajia kuvuna tani 1320 ikiwa ni ongezeko kubwa.
Akizungumzia suala la afya ya Udongo
Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba kujua hali ya udongo ni
jambo la muhimu ili kuwafanya wakulima wasiendelee na kilimo cha kubahatisha na
kuahidi kufanya kila jitihada ili kusaidia sekta ya kilimo.
Alisema alizungumza na wataalamu wa
udongo kutoka kituo cha utafiti Uyole ambao wamemweleza kuwa ardhi ya mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini inakabiliwa na udongo kuwa na tindikali nyingi hivyo
kufanya mbolea za chumvichumvi kutokuwa na tija, hata hivyo alisema wanaweza
kutumia chokaa kupunguza hali hiyo.
Hata hivyo alisema kutokana na kuwa
katika mkoa wa Songwe madini hayo ya chokaa yanapatikana kwa wingi wataalamu watafika
kukagua kama ndiyo yanayofaa kwa ajili ya kupunguza tindikali hiyo ya udongo
ili wakulima waweze kuitumia kutibu udongo.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Songwe
Luteni Mstaafu Chiku Galawa akizungumza katika kituo cha uzalishaji Mbegu
Magamba alikitaka kituo hicho kuongeza ubunifu ili kuweza kuwezesha wakulima
wadogo wadogo kujifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji wa mbegu na elimu
nyingine ili kueneza teknolojia ambayo itasaidia kupunguza tatizo la kuuziwa
mbegu bandia.
Alisema wakulima wa mkoa wa Songwe wana
uwezo mkubwa wa kulima lakini wanakwamishwa na changamoto ambazo hata hivyo
zikisimamiwa vizuri zinaweza kutatulika na kuwa kitendo cha mbegu kusafirishwa
kwenda kusindikwa Mbeya kinahamisha ajira za wakazi wa eneo hilo na ni kinyme
cha mkakati wa mkoa kuanzisha viwanda ili malighafi zinazozalishwa ziweze
kusindikwa katika eneo husika.
Awali katika taarifa yake Mkurugenzi
Mtendaji kiongozi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Firmin Mizambwa pamoja na kuwa
afya ya udongo kuwa tatizo linalopunguza ufanisi wa uzalishaji lakini pia
wakala huo unakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ukosefu wa umeme wa grid
ya taifa ambao unasababisha mbegu zinazozalishwa hapo kusafirishwa hadi Mbeya
kwa ajili ya kusindikwa hali ambayo inaongeza gaharama.
Mizambwa aliongeza kuwa pia wanakabiliwa
na tatizo la wananchi kuvamia shamba na uharibifu wa misitu ikiwa ni pamja na
mifugo kuingia kiholela kwenye shamba.
Stephano Simbeye, Mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)