ZIARA YA
WAZIRI MKUU MKOANI SONGWE
Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa alifanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe kuanzia tarehe 20 –
24/07/2017.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alitembelea miradi
mbalimbali. katika Wilaya ya Momba alitembelea mradi wa umwagiliaji wa
Naming’ongo, Ujenzi wa nyumba za Watumishi na kuzindua zoezi la upimaji ardhi
na kutoa Hati za Kimila. Halmashashauri ya mji wa Tunduma Mradi wa Kituo cha
pamoja cha ushuru wa Forodha (One Boarder Stop Post – OSBP), Ileje alizindua
ujenzi wa OPD. Kuzindua daftari la Wakazi la Kieletroniki (ambalo litatumika
kuanzia ngazi ya kitongoji, na kuzindua
kitabu cha Rasimu ya Mkoa wa Songwe.
Katika majumuisho alisema haya
Ulinzi na
usalama
Wananchi waendelee kushirikiana na vyombo vya ulinzi
na usalama wa wananchi katika mapambano dhidi ya mauaji ya wazee, Walemavu wa
ngozi – Albino, ulevi uliokithiri wa Viroba, mila zilizopitwa na wakati za
kunyima haki wanawake na watoto
Pembejeo
Feki
Alikemea swala la usambazaji wa pembejeo feki na kuwa
serikali hitafumbia macho na alitaka ushirikiano ili kudhibiti usambazaji wa
pembejeo feki
Aiongeza kuwa pembejeo zenye ubora zisambazwe kwa wakati. Uchumi
Waziri Majaliwa alisema kuwa Serikali itaendea
kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu
Uhakika wa
chakula
Waziri
aliwataka Wananchi wahakikishe wanakuwa na uhakika wa chakula kwa kupanga
bajeti ya mavuno ili kuepukana na balaa la njaa
Upimaji wa
ardhi
Wazari Mkuu
alitoa shukrani kwa mkoa wa Songwe kuzingatia umuhimu wa ardhi kwa kuanza kupima ardhi yake ili iongeze thamani na kuwa
na matumizi bora ya ardhi – kilimo, mifugo, hifadhi ya misitu, hifadhi ya
wanyama pori na kuwa hilo litapunguza migogoro isiyo ya lazima.
Afya
Wazir Majaliwa
alisisitiza umuhimu wa kuboreshewa huduma za Afya – Mama Wajawazito na Watoto
Elimu
Kutokana na serikali kutoa huduma za elimu bure Waziri
aliagiza ujenzi wa shule za ufundi ili kuongeza
ajira ya vijana
Vile vile kila
shule ianzishe madarasa ya awali ambayo yatatumika kuwaandaa watoto wa miaka minne hadi mitano kabla ya
kujiunga na darasa la kwanza.
Akijibia changamoto la uhaba wa Waalimu Waziri
Majaliwa alisema serikali imetoa vibali
vya ajira kwa watumishi 10,184 kuziba pengo la Watumishi Feki, na vibali
vingine 52,436 ambapo katika idadi hiyo wamo Watumishi wa Sekta ya Elimu.
Utalii
Waziri mkuu aliagiza kuwa Vivutio vya utalii viboreshwe
na kutangazwa ili kuongeza vyanzo vya mapato.
Ulevi
Waziri Mkuu Majaliwa alikemea tabia ya ulevi na kuzuia
usambazaji na matumizi ya pombe aina ya Viloba.
Hali ya
ulinzi na Usalama mipakani
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alitoa agizo kuwa waliojenga nyumba ndani ya mita 50
kutoka mpaka wa Tanzania na Zambia wabomoe
wenyewe katika muda wa siku.
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara baada ya kutembelea
mpaka huo aliagiza Halmashauri kuweka alama kwenye nyumba 250 ambazo
zilibainika kuwa ndani ya eneo huru (No man’s land) zinatakiwa kubomolewa kwa
muda usiozidi miezi mitatu.